Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametaja jumla ya majina 65 wanaotakiwa kufika kituo kikuu cha polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwaajili ya mahojiano.
Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari ofisini kwake asubuhi hii, Makonda alisema hiyo ni awamu ya pili baada ya majina ya awali yaliyowahusisha wasanii na askari polisi kuitwa polisi kwa ajili ya kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali.
Baadhi ya majina ya washukiwa hapo wanaotakiwa kuripoti polisi Februari 10 ni pamoja na Mbunge wa Hai, Freemani Mbowe, Mchungaji Josephat Gwajima na aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan.
Wengine ni Mmiliki wa Slipway, Yach Club, Mwinyi Machata, mmiliki wa Seacliff Casino, Husein Pambakali, wamiliki wote wa Casino, Kiiza, Chizega na wengineo.
2 comments:
Hii vita ya madawa ya kulewa inaendeshwa kimajungu zaidi ili kuwakomoa watu na kuwaharibia majina yao. Hamna mtu anayepinga vita vya madawa ya kulevya lakini approach wanayoitumia siyo nzuri. Unapomtangaza mtu hadharani kwamba anahitajika Polisi kusaidia uchunguzi wa Polisi kuhusu madawa ya kulevya unamjengea huyo mtu suspicion dhidi yake kutoka kwa jamii ya Watanzania. Jamii inaanza kumshuku hata kama hahusiki. Hata ikija kudhihirika kwamba huyo mtu siyo mhusika itakuwa ni kazi ngumu sana kumsafisha. Ndiyo maana Polisi siku zote wanafanya uchunguzi wao kwa siri na wanapopata ushahidi ndipo wanapomfungulia mashtaka mtu na hata kuweza kutangazia umma kwamba fulani anahusika na madawa ya kulevya au amekamatwa nazo.
Lakini hili zoezi sasa hivi inaendeshwa kisiasa zaidi ili kumjengea umaarufu Mkuu wa mkoa wa Dar ew salaam Bwana Paul Makonda. Lakini haifuati maadili wala miiiko katika kuwachunguza watuhumiwa. Kwanini Mkuu wa mkoa asifanye uchunguzi kwa siri halafu akishapata uthibitsho (siyo tetesi) awafungulie mashitaka wote wanaotuhumiwa? Kwa sababu jinsi ilivyo sasa hivi akisikia rumours kuhusu mtu au sehemu kunakosemekana kwamba madawa ya kulevya yanauzwa. Yeye anawaita hawa watu na wamiliki wa hayo maeneo kupitia vyombo vya habari. Hii si sawa. Kwanza ukimtangaza mtu unayemshuku anatumia au anayeuza madawa ya kulevya na ukampa siku kadha afike Polisi kwa mahojiano unakuwa unampa muda na nafasi ya kutosha na upenyo wa kuyatupa, kuyaficha au kuyaharibu hayo madawa ya kulevya.
Kwa hiyo kinachotakiwa ni kuiendesha hii campaign kwa kujali utu wa watu na hasa wale wanaoshukiwa pasipo kuwepo na ushahidi kwa sababu kama hawana hatia watakuwa wameharibiwa majina yao na sifa zao katika jamii pamoja na adha kubwa ambao watakuwa wameipata kwa kuhusishwa na hii campaign ya kutokomeza madawa ya kulevya.
Acheni Makonda afanyekazi yake. Kwa atakaeona amedhalilishwa for false accusations amfungulie kesi Makonda cha ajabu mpaka sasa kila mtu analalakia kwenye media tu.
Post a Comment