ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 16, 2017

TANZANIA ITAENDELEA KUWA MWENYEJJI WA PROGRAMU YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA.

 Mwenyekiti  wa Programu ya  Urithi wa Ukombozi   wa  Bara la Afrika  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa maelezo kuhusu Programu hiyo kwa wajumbe katika kikao kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha mchango wake kwa wajumbe  wakati wa kikao cha Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu wa Programu  ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Dkt Daniel Ngagala akiwasilisha mada wakati wa  kikao na wajumbe wa Programu hiyo kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi akichangia mjadala wakati wa kikao cha Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akiwasilisha mchango wake katika kikao cha Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wataalamu wa Program ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika wakiwasilisha mawazo yao katika kikao cha Programu hiyo kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawaziri na manaibu Mawaziri,Viongozi  na Wajumbe wengine wa Program hiyo baada ya kumaliza kikao kilichofanyika jana Jijini. Dar es Salaam.

1 comment:

Anonymous said...

Nnaimani wakati umefika Tanzania kuwa kiongozi wa ukombozi wa bara la Africa kiuchumi vile vile, hakuna lisilo wezekana. Ikiwa tulijotolea mhanga kuhakikisha Africa inatoka kwenye mikono ya wakoloni vipi tushindwe katika mapinduzi ya kiuchumi? La msingi ni kutangaza vita rasmi juu ya kupambana na umasikini na iwe serious kuliko vita ya kumuondoa mkoloni wakati ule nnaimani kwa njia hii tutafika mapema. Watanzania tunauchukulia umasikini kimzaha mzaha kama vile ndio asili yetu kitu ambacho ni upumbavu wa akili. Tunatakiwa kuwa aggressive kama tulivyokuwa tukipigania uhuru wa bara la Africa ili kujiondoa katika maisha duni ya kiuchumi lakini inaonekana baada ya Africa kuwa huru kiutawala tulidhani tumemaliza kazi na pengine tulitegemea kurejeshewa fadhila kutoka nchi tulizotumia rasilimali zetu nyingi ikiwemo rasilimali watu kuzipigania ili ziwe huru lakini ukweli ni kwamba kazi ndio ilikuwa inaanza ya kuijenga Tanzania baada kubweteka. Magufuli kaanza vizuri lakini hakuna vita ya serikali itakayopata mafanikio bila kuungwa mkono na wananchi waliowengi kwa hivyo vita ya kampeni ya kuwaelimisha watanzania juu ya kuondokana na umasikini kwa njia halali iwe kubwa zaidi kuliko ilivyo sasa. Kwa hivyo kimsingi Africa ikiwa bado hatuwezi kujitegemea katika kuendesha serikali zetu mpaka kwa misaada kutoka nje waafrica hatuja komboka bado na tunatakiwa kukaa chini ili kujielimisha zaidi nini maana ya ukombozi?