ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 28, 2017

TNRFwakishirikiana na TALA wazindua mpango mkakati wa kitaifa wa kuboresha usimamizi na utawala wa Ardhi Tanzania

Kamishna wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo(aliyesimama) akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi hapa nchini Tanzania ambao utajumuisha mradi wa majaribio katika mikoa mbalimbali kuona kama utawezekana maana swala la upatikanaji wa ardhi imekuwa ni changamoto kubwa sana hapa nchini.

Mpango mkakati huu kwa Tanzania unatekelezwa na Asasi za kiraia ikishirikiana na serikali ya Tanzania, unafadhiliwa na International Land Coalition(ILC), Irish Aid, International Food for Agriculture Development(( IFAD) na kuratibiwa na Tanzania Land Alliances( TALA). 
Mkurugenzi wa Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Joseph Olila akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi hapa nchini Tanzania  ulioratibiwa na TALA ili kuweza kupatikana kwa ardhi hasa maeneo ya vijijini.
Mkurugenzi Mtendani wa Taasisi ya MVIWATA ya Morogoro, Steven Ruvuga akizungumza jinsi wanavyoweza kuhamasisha watu kwenye matumizi mazuri yaardhi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi kwenye mkutano uliofanyika kwneye ukumbi wa Hotel ya Wanyama jijini Dar es Salaam.
Bwana Alain Essimi Biloa kutoka International Land Coalition(ILC) akitoa mada juu ya matumizi mazuri ya ardhi kwenye jamii hasa kwa wananchi waishio vijijini.
Baadhi ya wadau wakichangia mada kwenye kongamano lililofanyika leo katika Hotel ya Wanyama jijini Dar es Salaam leo
Baadhi ya wadau wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi unaoratibiwa na Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF).
Meneja Program wa Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Zakaria Faustine akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi hapa nchini Tanzania.
Afisa Program za Ardhi Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF),Godfrey Massay akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkakati waliojiwekea kama Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Kamishna wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kufanya uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi utakaoleta tija kwa wananchi hasa vijijini.
Picha ya Pamoja

No comments: