Tangazo hilo linafuatia misururu kadhaa ya tweeter kutoka kwa Trump, ambapo anampinga jaji aliyetoa uamuzi huo, huku akionya kuwa watu wabaya na hatari, huenda wakamiminika hadi Marekani kutokana na uamuzi huo.
Mashirika makubwa ya usafiri wa ndege, yangali bado yanawakubalia raia kutoka mataifa hayo husika, kuabiri ndege na kuingia Marekani.
Kumekuwepo na maandamano dhidi ya marufuku hiyo ya Trump huko Washington, jimbo la Miami na miji mingine kadhaa ya Marekani, pamoja na miji mingine mikuu ya bara Ulaya.
Wakati huo huo, Rais Trump ametetea uhusiano wake na Rais Vladimir Putin, katika mahojiano ya Runinga, huku akikataa kupinga madai ya mtangazaji kuwa Rais huyo wa Urusi ni muuaji.
Katika mahojiano ambayo yatapeperushwa na runinga ya Fox News baadaye leo Jumapili, Bwana Trump ameashiria kuwa Marekani isijifanye kutokuwa na hatia, kwani pia ina wauaji wengi.
Amesema kuwa anamheshimu Bwana Putin, na itakuwa jambo bora zaidi ikiwa Urusi itasaidia Marekani kupambana na wanamgambo wa kundi la Islamic State.
No comments:
Post a Comment