ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 23, 2017

UJUMBE WA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA - NDC WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA MAGEREZA, JIJINI DAR


Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(meza kuu) akiongea na ujumbe kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa. Ujumbe huo wa Washiriki wa Mafunzo wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa shughuli za Magereza hapa nchini leo Februari 23, 2017.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akisisitiza jambo kwa Maafisa kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) walipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa Jeshi hilo.

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akitoa utambulisho mfupi kwa Wakufunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania alioambatananao katika ziara ya mafunzo.



Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo hayo kama inavyoonekana katika picha

Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakipata maelezo mafupi toka kwa Wataalam wa Jeshi la Magereza walipofanya ziara ya mafunzo katika Kiwanda cha Seremala Gereza Kuu Ukonga, Dar es Salaam leo Februari 23, 2017.

Kamishna Msaidizi wa Magereza, Charles Novart akiwasilisha mada yake ya uchokozi kuhusu Historia na Muundo wa Jeshi la Magereza mbele ya Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania(hawapo pichani).

Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakifuatilia mijadala katika uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam leo Februari 23, 2017.

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akikabidhi zawadi kwa Naibu Kamishna wa Magereza, Edith Mallya(kushoto) mara baada ya uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam leo Februari 23, 2017.

Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa(wa sita toka kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania walipofanya ziara ya mafunzo waliyoifanya katika Jeshi la Magereza(wa nne toka kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments: