Wednesday, February 15, 2017

WATANZANIA 132 WARUDISHWA KUTOKA MSUMBIJI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Suzan Kolimba 

Idadi ya Watanzania waliofukuzwa Msumbiji imeongezeka mpaka kufikia 132, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka zaidi kutokana na operesheni ya kuwarudisha nyumbani wahamiaji haramu.
Akizungumzia suala hilo leo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Suzan Kolimba amesema operesheni hiyo haijawalenga Watanzania pekee bali raia wa nchi nyingine walioingia Msumbiji kinyume cha utaratibu.
Dk Kolimba amesema mji wa Montepuez uliopo jimbo la Cabo Delgado una Watanzania 3,000 wanaoishi huko na kwamba idadi ya watakaoondolewa inaweza kuongezeka zaidi.
"Tunaendelea kufuatilia tuhuma za baadhi ya Watanzania kwamba walifanyiwa ukatili wakati wanarudishwa nyumbani ili tujue hatua za kuchukua. Maofisa wetu wanashirikiana na serikali ya Msumbiji katika kuhakikisha Watanzania hawapati matatizo katika operesheni hiyo," amesema.

No comments: