ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 10, 2017

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTEMBELEA KITUO CHA PEDDEREF SOBER HOUSE KIGAMBONI

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi akitoa nasaa kwa wanawake na vijana walioathirika na janga la madawa ya kulevya kituoni hapo mapema leo asubuhi.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi akimpa mkono wa pongezi mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe kwa jitihada anazoendelea kuzifanya katika kuhakikisha waathirika wote wa madawa ya kulevya waliopo kituoni kwake wanapata elimu ya kutosha na hatimaye kuacha kabisa utumiaji wa madawa hayo.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi (kushoto) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa kituo People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef), Nuru Salehe wakati wa sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani mapema leo asubuhi. Kulia ni Jacqueline Samson na Ashura Diwani.
Moja ya wanawake waathirika wa madawa ya kulevya bi. Jacqueline Samson aliyesimama (katikati) akitoa shukrani kwa viongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambao hawapo picha kwa kuwatembelea kituoni hapo pia kwa msaada waliowapatia.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jennifer Shirima ambaye aliambatana na msemaji wa Jeshi hilo katika ziara hiyo akiwasisistizia wanawake hao kutoajiingiza tena kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya na kuwakumbusha kuwa “Wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi” (kulia) ni Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe na (kushoto) ni Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi ambaye pia ni msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Maafisa na Askari (Wanawake) wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Mkurugenzi wa People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef) bi. Nuru Salehe wa kwanza mbele (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliopata kuathirika na madawa ya kulevya kituoni hapo, ambapo wanawake hao wameanza kurejea katika hali zao za kawaida mara baada ya kupewa elimu na malezi yanayostahili.

Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeungana na wanawake duniani kuadhimisha siku hiyo.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi alisema katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano (5) kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya, kupitia Jeshi hilo Nzalayaimisi aliwaongoza Askari (wanawake) kutembelea kituo cha Pedderef Sober House na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.

Ambapo aliiomba jamii isiwanyanyapae pamoja na elimu wanayoendelea kuipata kituoni hapo ameiasa jamii kujitokeza kuwasaidia na kuwawezesha kwa hali na mali ili waweze kujiajili wenyewe kwani wanapotoka kituoni hapo wanakuwa hawana uwezo wakujiajili na kujikuta wanarudia tena kwenye janga la madawa hayo.

Pia Nzalayaimisi aliendelea kusema kwa kutoa pongezi kwa serikali na wadau mbalimbali wote waliojitokeza na kuthubutu kufanya maamuzi ya kujitoa katika kupambana na janga hilo na pia alimpongeza mkuu wa mkoa wa dar es salaam paul makonda kwa kuongoza mapambano hayo. 

Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe naye alisema napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa msaada wao wa hali na mali waliotupatia na kuomba taasisi nyingi na wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia kituo hiki kwani wengi wamenufaika kutokana na elimu na malezi wanayoendelea kuyapata kituoni hapo.

No comments: