ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 10, 2017

TCCIA INVESTMENT PLC YATOA DARASA KWA WAKAZI WA LINDI NA MTWARA KUHUSU SOKO LA HISA.

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya TCCIA Investment PLC bi Magdalena Mkocha akizungumza na wafanyabiashara mkoani Lindi katika ukumbi wa Double M humo.Bi Mkocha alisema TCCIA Investment ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na mtaji wa shilingi Bilion 1.97 imeweza kukuza mtaji hadi zaidi ya Bilion 28.6 na imekuwa ikilipa gawiwo kwa wanahisa wakeMkochi ameongeza kuwa TCCIA Investment PLC ni kampuni ya uwekezaji wa pamoja, imara na imekuwa ikifanya vizuri sana hivyo amewahimiza wajasiriamali hao kuitumia fursa hii muhimu na adhimu kabla ya March 14 mwaka 2017, ambapo milango ya uuzaji wa hisa hizo itafungwa
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Chemba ya Biashara,viwanda na kilimo, Magdalena Mkocha, amewataka wananchi na wafanyabiashara wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa ya soko la hisa za TCCIA Investment PLC kwa awamu ya awali ambayo inakaribia kuisha.
Hayo ameyasema wakati akizungumza wafanyabiashara kwenye ziara yake ya mikoa ya kusini, Lindi na Mtwara alipokuwa kwenye mikutano ya kuhamasisha ununuzi wa Hisa hizo ambazo zinamilikiwa na kampuni hiyo.
Bi Magdalene Mkocha akifafanua jambo kwa wafanyabiashara waliohudhulia mkutano huo mkoani Lindi
“Nipende kuwahimiza ndugu zangu tuchangamkie fursa hii kwasababu TCCIA Investment PLC nikampuni imara ambayo imeweza kusimama na kujiendesha yenyewe kwa kipindi kirefu bila kutegemea mikopo, sasa imeona ni wakati sasa kuwapa na wananchi nafasi ya kushiriki katika kuchangia mitaji yao ili mwisho wa siku wavune matunda kupitia hisa zao” alisema Bi Mkocha
Mmoja wa wajasiriali waliohudhulia mkutano huo Bwana Condrad Makwiya akiuliza swali kwa bi Mkocha kuhusiana na upatikanaji wa hisa hizo
Hisa za TCCIA Investment PLC zinapatikana kwa shilingi 400 tu, huku kima cha chini cha kununua hisa hizo kikiwa ni hisa 100, pia unaweza kupata hisa hizo kupitia kwa mawakala wa walioidhinishwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) au tembelea kwenye matawi yoyte ya Benki ya CRDB.
Pia unaweza kutumia simu ya mkononi kwa kupiga *150*36# kisha kufuata maelekezo.
Bi Madgalena Mkocha akigawa vipeperushi kwa wafanyabiasha mkoani Mtwara baada ya kumalizka kwa mkutano huo kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Mtwara.
Moja ya mshiriki mkoni Lindi akitoa shukrani zake kwa uongozi wa TCCIA Investment PLC kuhusu fursa hiyo uuzaji wa hisa

No comments: