ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 10, 2017

KIKAO MAALUM CHA BARAZA KUU LA UVCCM CHA RIDHIA NA KUPITISHA MAPENDEKEZO YA MAREKEBISHO YA KANUNI YA UVCCM

Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika kikao cha kamati ya Utekelezaji kilichoketi mapema ya leo kabla ya kikao cha Baraza kuu Maalum la Uvccm Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma.
Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Sadifa Juma Khamis wa pili kulia akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alipowasili katika kikao cha Baraza kuu Maalum la Uvccm Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma.
 Mwenyekiti Wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg:Sadifa Juma Khamis akifungua Kikao cha Baraza Kuu Maalum la UVCCM Taifa kilichofanyika Mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Mohammed Seif Khatibu Akizungumza  katika kikao  cha Baraza kuu Maalum la Uvccm Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma leo.
Ndg:Nyundo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kupitia UVCCM akichangia hoja katika kikao cha Baraza kuu Maalum Kilichofanyika leo Mjin Dodoma.
Mhe: Deo Ndenjembe Mkuu wa Wilaya ya Kongwa akichangia hoja katika kikao cha Baraza kuu Maalum Kilichofanyika leo Mjin Dodoma.
 Wajumbe Wa Baraza kuu la UVCCM Taifa
 Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mariam Ditopile akisikiliza kwa Makini
  Wajumbe Wa Baraza kuu wakiwa kikaon
SOMA

MAAZIMIO YA BARAZA KUU MAALUM LA UMOJA WA VIJANA WA CCM TAIFA LILILOKUTANA ALHAMIS TAREHE 9/03/2017 ROYAL VILLAGE HOTEL MJINI DODOMA

Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo Alhamis tarehe 9/03/2017 umefanya kikao cha Baraza Kuu la UVCCM Taifa Maalum chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Sadifa Juma Khamis (MCC)(MB) katika Hotel ya Royal Village Hotel Mjini Dodoma.

Kikao kwa kauli moja kimepitisha na kuridhia mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni ya Umoja wa Vijana wa CCM kufuatia maboresho ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi Toleo la 1977 marekebisho ya 2017 na kupeleka katika Vikao vya Chama Cha Mapinduzi Taifa kwa hatua zinazoendelea.

 “Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itakuwa na uwezo kwa kushauri, kutoa maagizo ya jumla na maelekezo maalum kwa Jumuiya zinazoongozwa na CCM”.

“Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itathibitisha Kanuni/Katiba ya kila Jumuiya inayoongozwa na CCM marekebisho yake kabla ya kutumika”. Katiba ya CCM ya 1997 Toleo la 2012 uk. 191 kifungu (4) na sura ya (5).

Kufuatia kikao   Maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM na kuzingatia mambo yafuatayo:-

Mabadiliko ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake yana lengo la kukiimarisha Chama chetu ili kuzidi kuziteka hisia, mioyo na fikra za Watanzania walio wengi kwa nia ya kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika lengo lake la kushika dola na kuleta maendeleo endelevu.
Kupunguza idadiya wajumbe ili kuwa na michango makini kwenye vikao vyetu ili kuweza kuwajengea na kuwatetea Vijana wakulima na wafanyakazi na wale walio katika sekta binafsi ili wanufaike na masuala ya Kiuchumi, kijamaii na Kisiasa kulingana na fursa zilizopo kama zilivyoainishwa na kuelekezwa na sera za CCM katika misingi ya kujitegemea.

Mabadiliko haya yatasaidia sana kupunguza migogoro isiyo na msingi katika Jumuiya inayotokana na Vikao vya Kikanuni.

Aidha Umoja wa Vijana wa CCM unaahidi kwa CCM kufanyia kazi maagizo na maelekezo yote yatakayotolewa kwa lengo la kufikia kwa vitendo dhana ya CCM mpya, Tanzania mpya wakati Jumuiya hiyo ikielekea kutimiza miaka 40 toka kuzaliwa na kumepiga hatua kubwa za mafanikio Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.

Mwisho UVCCM imempongeza kwa dhati Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa umakini, uhodari, ushupavu na kusimamia vyema Ilani ya Uchaguzi wa CCM sambamba na azma yake ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.

PICHA NA FAHADI SIRAJI

1 comment:

Anonymous said...

huyu mtu lemutuz ( William Malechela) anafanya nini kwenye kikao hiki wakati jamaa ni miaka karibu 60. Ufisadi mtupu.