Mbunge
wa Arusha mjini Godbless Lema akizungumza na wananchi katika mkutano
wa hadhara uliofanyika shule katika viwanja vya Ngarenaro Jijini
Arusha.
Wapili kutoka kushoto ni mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema
,wakwanza kulia ni mbunge wa Simanjiro James OLemilya akifuatiwa na
aliyeko kulia kwake ni Meya wa jiji la Arusha Kalisti
Lazaro, akifuatiwa na Wema Sepetu,na wakwanza kulia ni mwenyekiti wa
CHADEMA mkoa wa Arusha Derick Magoma
Wema Sepetu akisaliamia wananchi wa jiji la Arusha waliofika kwenye mkutano huo
Mamia
ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo jijini
Arusha.
Na,Vero Ignatus ,Arusha.
Mbunge wa
Arusha mjini Godbless Jonathan Lema amefanya mkutano wake wa kwanza
kwa kuzungumza na wananchi wa Arusha baada ya kutoika rumande
alipokuwa ameshikiliwa kwa miezi minne
Akizungumza katika mkutano huo Lema amesema kuwa madiwani
wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema watakao kuwa waoga yupo
tayari kuwakana mbele ya wananchi na kama hawawezi kuwa majasiri
waachanae na chama hicho.
Mkutano
huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo
madiwani wote wa chama hicho katika jiji la Arusha pamoja na wabunge
wa simanjiro na yule wa Monduli.
Aidha
mbunge huyo amesema kuwa yupo kwenye harakati za kukamisha kukiandika
kitabu chake kitakachotoka hivi karibuni chenye historia ya maisha
halisi ya wafungwa waliopo gerezani bila hatia,sambamba na wale
waliobambikiziwa kesi mbalimbali.
Ameataka
madiwani kuwa sambamba na yeye na kuachana na kauli wanayoisema ya
kuwa wapo nyuma yake kwa kila kitu anachokifanya .
No comments:
Post a Comment