Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa amesema anawakaribisha Chadema waliofukuzwa uanachama baada ya mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitisha uamuzi wa kuwatimua 12 kati ya 24 walioadhibiwa.
Amesema walioadhibiwa ni mashujaa waliosimama kutetea demokrasia.
Lowassa yuko katikati ya tuhuma zilizosababisha wanachama wengi wa CCM kuchukuliwa hatua baada ya uamuzi wake wa kuhamia Chadema kupinga kuenguliwa kugombea urais, kufuatiwa na viongozi kadhaa na wanachama kujiondoa chama tawala na kujiunga na upinzani.
Katika taarifa yake aliyoituma kwa vyombo vya habari jana, Lowassa ambaye pia alikuwa mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM hadi mwaka 2015, amesema viongozi waliotimuliwa na chama hicho tawala walitumia demokrasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria.
“Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki, demokrasia na taratibu na kupinga dhuluma ndani ya chama chao na nchini,” amesema Lowassa, ambaye kabla ya kuenguliwa alikuwa mmoja wa makada waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kupitishwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM.
2 comments:
Ok its ok kuwakaribisha but kama hawa walikuwa wanapinga why hawakutoka all that time mpaka kufukuzwa.As tumeshaona walio toka CCM na baada ya uchaguzi kuisha wamesharudi CCM ....so kuweni makini watu mnaowapokea simetimes.
Ukawa na Chadema hawana principles. Watu wanafukuzwa hata kwa tuhuma za madawa ya kulevya hakuna busara ya kusema tusubiri ushahidi? Yeyote yule bila kujali kwanini amefukuzwa ili mradi katoka CCM anapokelewa tu!!! What a shame. Ndiyo shida ya kupokea viongozi mamluki. Vyama vya namna hii haviendi mbali.
Post a Comment