Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi pamoja na Wakuu wa Vyombo vilivyo chini ya Wizara yake mkoani humo. Katika mzungumzo hayo, Masauni aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuanzisha Kituo cha Zimamoto wilayani hapo kuanzia mwezi Aprili mwaka huu pamoja maandilizi ya Ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi wilayani humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Fundi Mkuu wa ujenzi wa Gereza Ruangwa (kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo unaoendelea mjini Ruangwa. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Lindi, Tusekile Mwaisabila.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ruangwa, Joseph Kiyengi wakati alipokuwa akionyesha eneo litakalojengwa Kituo kipya cha Polisi wilayani humo. Maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho yameshaanza. Katika ziara yake Masauni pia aliagiza uanzishwaji wa Kituo cha Zimamoto wilayani humo haraka iwezekanavyo. Katikati ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Twaha Mpembenwe.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ruangwa, Joseph Kiyengi alipokuwa anatoa taarifa yake katika Kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ruangwa ambacho kilijumuisha Wakuu wa Vyombo vilivyo chini ya Wizara hiyo mkoani Lindi. Katika mzungumzo hayo, Masauni aliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuanzisha Kituo cha Zimamoto wilayani hapo kuanzia mwezi Aprili mwaka huu pamoja maandilizi ya Ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi wilayani humo.
No comments:
Post a Comment