ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 29, 2017

Messi afungiwa mechi nne Argentina

Lionel Messi amefungiwa mechi nne za kimataifa saa tano kabla ya mchezo wao wa jana usiku na Argentina wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Bolivia.

Kiungo huyo mshambuliaji wa Argentina na Barcelona alishushiwa adhabu hiyo kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi wa pembeni wakati wa mchezo wao wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chile.

Messi, ambaye alifunga bao pekee katika mchezo huo, alishikwa na hasira wakati mshika kibendera liponyoosha kuashiria kuwa nahodha huyo alicheza rafu, kitendo kilichomfanya amshushie maneno.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 29 sasa, pia alipigwa faini ya Pauni 8,100 sambamba na adhabu hiyo ya kutoichezea Argentina mechi nne.

Kutokana na adhabu hiyo, Messi atakosa mechi nne zijazo za taifa lake.

Argentina inashika nafasi ya tatu katika kundi lao la Amerika Kusini la kufuzu, wakati timu nne za juu ndizo pekee zitakazopata nafasi ya kucheza fainali zijazo nchini Urusi.

Hadi sasa, kundi hilo limebakiza mechi tano kwa za mwisho za kutafuta nafasi hiyo.
MWANANCHI

1 comment:

Anonymous said...

Mwandishi, Argentina inashikilia nafasi ya Tano na siyo ya Tatu katika kundi South America. Brazil, Colombia, Uruguay, na Chile ni Top Four teams. Kuna hatari Argentina itakosa safari ya Urusi 2018.