Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Chama cha Democrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani Mhe. Frederick Sumaye ameiomba serikali kusimamia misingi ya demokrasia katika kutatua malalamiko ya wananchi na kusimamia ustawi wa jamii ya Watanzania.
Mhe. Sumaye ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kama serikali itafanyia kazi malalamiko na mapendekezo yanayotolewa na wananchi ni wazi taifa litafikia malengo yake iliyojiwekea ya kupunguza hali ya umasikini na kuongeza pato la taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo Mhe. Sumaye amewaasa watendaji wa serikali kutumia vizuri misaada inayotolewa na nchi wahisani ili kuhakikisha fedha za wananchi zinazotumiwa katika ulipaji wa madeni hayo zinakuwa na manufaa kwa watanzania wote hasa wale wasiofikiwa na huduma muhimu za kijamii.
Credit:EATV
1 comment:
Leo Sumaye ndie anajua kutoa ushauri! kwani ulipokua kiongozi zile pesa mlikua mnazifanyia nini. Watu wengine mlitakiwa kupotea bongo kama ulivyokuja kujificha Harvard University ukidai umekuja kusoma kumbe ulikimbia skendo. Mimi naona serekali iko sawa bila ushauri wako maana hata wewe ulishindwa kufuata ushauri unaowapa wenzio ukajitajirisha ukasahau maskini. katika orodha ya watu waliohujumu uchumi na wewe umo. so be silent please
Post a Comment