TAARIFA:
SHIRIKA
la Umeme Nchini (TANESCO) linakanusha Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maji
Safi na Maji taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), kuhusu kukosekana kwa Huduma
ya maji kwa siku ya Jumapili tarehe
12/03/2017 kwa wakaazi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ili kupisha TANESCO kufanya matengenezo ya
ukamilishaji kazi ya kuunganisha umeme kwenye
mtambo mpya wa maji wa Ruvu Juu.
Aidha,
Taarifa hiyo ya DAWASCO iliainisha kuwa ukosefu huo wa Huduma ya maji unatokana
na matengenezo yatakayofanywa na TANESCO kwa siku husika.(12/03/2017).
TANESCO
inapenda Umma ufahamu yafuatayo;
Mosi, TANESCO ilipokea ombi la DAWASA kupitia Mkandarasi wao (M/s Mollel
Electrical Engineering) wiki iliyopita la kuomba kuzimwa umeme ili wakamilishe
kazi ya mradi wa kuongeza mashine za kusukuma maji kwenye kituo cha Ruvu juu
kilichopo Mlandizi, kupitia mradi huo mashine nne zinazohitaji megawati 2 kila
moja zimefungwa
Wataalam
wa TANESCO waliishauri DAWASA wajenge laini ya kilovolti 33 kutoka Chalinze
hadi Mlandizi ili kuzipatia umeme mashine
hizo mpya walizoongeza.
Pili, Baada ya wataalam wa TANESCO kutembelea eneo
hilo na kufahamu uharaka wa mradi huo wa maji kwa Wananchi ilishauri DAWASCO
kwa barua kuwa umeme uzimwe siku ya ijumaa tarehe 10/03/2017 ili Mkandarasi wa
DAWASCO
kufanya kazi hiyo, ushauri ambao DAWASCO iliupinga wakiomba umeme uzimwe siku ya Jumapili tarehe 12/03/2017 ili wapate muda wa kuwaarifu Wateja wao na TANESCO iliridhia.
kufanya kazi hiyo, ushauri ambao DAWASCO iliupinga wakiomba umeme uzimwe siku ya Jumapili tarehe 12/03/2017 ili wapate muda wa kuwaarifu Wateja wao na TANESCO iliridhia.
TANESCO
imeshangazwa na Taarifa hiyo ya DAWASCO kuwa TANESCO inafanya matengenezo
ambayo yatapelekea ukosefu wa huduma ya maji huku ikitambua TANESCO inatekeleza
ombi lao walilolileta.
Tunasisitiza
kuwa, taarifa za TANESCO kufanya
matengenezo si za kweli na uzimaji umeme siku ya Jumapili tarehe 12/03/2017 ni
kwa ajili ya kupisha Mkandarasi wa DAWASCO kufanya kazi kama walivyoomba
na si TANESCO.
Imetolewa
na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu.
2 comments:
Hivi hizi tofauti zisingeweza kuwa sorted out quietly bila kuzua hii drama? Haya mashirika yetu yote ovyo tu.
Think about it, TANESCO paid for this announcement!!! That it is absurd says little!!! DAWASCO too revealed the mysteries surrounding management of our public institutions ... rarely used to transparency and honesty..... aluta continua
Post a Comment