NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme Tanzania, (TANESCO), limetoa siku 14 kwa Wateja wake wote linalowadai
kulipa madeni yao, vinginevyo litasitisha utoaji wa huduma ya nishati kwa
wahusika.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari leo Machi 9, 2017 ofisini kwake jijini Dar es
Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (pichani juu), alisema, Shirika
linadai jumla ya shilingi Bilioni 275.38.
Akifafanua
zaidi alisema, Wizara na Taasisi za Serikali zinadaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni
52.53, Shirika la Umeme Zanzibar, (ZECO), linadaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni
127.87, na Makampuni binafsi na wateja wadogo wadogo deni ni zaidi ya Shilingi
Bilioni 94.97.
“Zoezi
hili litaambatana na utoaji taarifa (notice) kwa wadaiwa wote kulipa madeni yao
ndani ya kipindi cha siku 14, baada ya hapo Shirika litachukua hatua ya
kusitisha Huduma kwa Wateja watakaoshindwa kuanza kulipa madeni yao pamoja na
hatua zingine za kisheria.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Aidha,
alisema kwa wale wateja wadogowadogo, Shirika halitawaandikia barua kwani ni
wengi, isipokuwa kupitia ofisi ya Uhusiano ya Shirika, wataarifiwa kupitia
vyombo vya habari.
Alisema
Malimbikizo hayo ya madeni yamekuwa yakikwamisha jitihada za utekelezaji wa
majukumu mbalimbali ya msingi ndani ya Shirika kwa wakati, ikiwemo shighuli za
Uendeshaji Shirika, Matengenezo ya Miundombinu pamoja na utekeelzaji wa miradi
mbalimbali.
“Ni
matarajio ya Shirika kuwa kuli[wa kwa malimbikizo haya ya madeni, kutasaidia
TANESCO kujiendesha kiushindani na kwa ufanisi mkubwa zaidi na hivyo kuendelea
kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme hapa
nchini.” Alihitimisha Dkt. Mwinuka.
Taarifa
hii ya TANESCO imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, kuliagiza Shirika hilo, kuwakatia umeme wale wote wanaodaiwa ikiwemo
taasisi nyeti za Serikali na hata Zanzibar.
Rais
alitoa agizo hilo wakati akizindua ujenzi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha
kupoza na kusambaza umeme wa Kilovolti 132 mkoani Mtwara ambacho kitaboresha
upatikanaji wa umeme kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi.
Baadhi ya viongozi wa TANESCO, kutoka kushoto, Dudu Fuime, (Kaimu Meneja Mwandamizi TEHAMA), Mhandisi Kahitwa Bishaija,(Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji umeme), Mhandisi Theodory Bayona,
(Meneja
wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme)
na Renata Ndege, (Afisa Mkuu wa Fedha) wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa mkutano huo
Baadhi ya viongoziwa juu wa TANESCO na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
Dkt. Mwinuka akiondoka ukumbini baada ya kutoa taarifa hiyo. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha wa TANESCO, Renata Ndege
No comments:
Post a Comment