ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 21, 2017

TOVUTI MPYA YA HABARI INAYOENDESHWA NA VIJANA WENYE NDOTO ZA UANDISHI WA HABARI

KUHUSU 360.com – TOVUTI INAYOENDESHWA NA VIJANA WENYE NDOTO ZA UANDISHI WA HABARI
Habari. Napenda kuchukua fursa hii kuwatambulisha tovuti mpya ya habari nchini Tanzania na duniani – www.360.co.tz
Tovuti hii ni maalum kwa vijana wote wa kitanzania ambao wana ndoto za kufanya kazi kwenye chombo fulani kikubwa cha habari.
Kupitia tovuti hii, vijana wajitoleaji kwenye tasnia ya habari, watatumia uwezo, ujuzi, na vipaji walivyo navyo kutengeneza habari, kuzihariri na kuzisambaza kwa ajili ya umma.
Hii ni nafasi pekee ambayo kijana mpenda habari anaweza kuitumia kupata uzoefu katika tasnia nzima ya habari, kwa kujitolea huku akiendelea kujijengea CV yake.
Kutuma habari kupitia www.360.co.tz ni bure, hakuna gharama yeyote na habari itawekwa kwa jina lako ili uendelee kujijengea jina na CV yako.
www.360.co.tz inapokea makala za aina zote, zilizochambuliwa vizuri na wataalamu mbali mbali. Pia itatoa nafasi kwa yeyote mwenye wazo ambalo anafikiria kuliweka mbele ya jamii, kulizungumzia wazo yake.
Pia, www.360.co.tz itakuletea matangazo ya matukio (events) mbali mbali yanayotokea nchini Tanzania kwa ajili ya vijana wa kitanzania. Tuma maelezo ya tukio lako na sisi tutayaweka kwenye tovuti hii bure kabisa.
Leo, tukizundua rasmi tovuti hii – www.360.co.tz ina wachangiaji takribani 20 ambao wako tayari kukuleta taarifa kiganjani kwako masaa 24 ya siku, siku 7 za wiki.
Sambaza ujumbe huu uwafikie vijana wengi iwezekanavyo wenye ndoto za uandishi wa habari ili wapate fursa ya bure kujifunza na kujaribu ujuzi wao kwenye tasnia hii. Ningependa ifahamike kuwa, tovuti www.360.co.tz haitengenezi faida yeyote kwa kusaidia vijana wapenda uandishi wa habari kujaribu taaluma yao.
Karibu www.360.co.tz mtandao usio na makuu wala vipingamizi vyovyote kwa mpenda habari duniani. Kwa mawasiliano zaidi, unaweza kutuma email kwenda 360habari@gmail.com
Imetolewa na:
Allan Lucky
Mwanzilishi wa www.360.co.tz
Simu: +254724805536

No comments: