Viongozi wa chama cha Demokarasia na Maendeleo wilaya ya Njombe wametoa maazio ya kuto fanya kazi na mkuu wa wilaya ya Njombe ,Bi RUTH MSAFIRI kwa kile walichodai kuwa alimdhalilisha mwenyekiti wa mtaa wa Buguruni kwa kumchapa makofi February 28 mwaka huu akiwa ofisini kwake.
Uongozi wa cham a hicho wilaya umekuja na tamko la pamoja na kumtaka mkuu wa wilaya a N jombe kuomba radhi ndani ya siku 7 na la sivyo hatapewa ushirikiano na vingozi wote wa chama hicho wakiwemo Wenyeviti wa Mitaa na Madiwani.
Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi, RUTH MSAFIRI amekana kumpigia mwenyekiti huyo na kusisitiza aliamuru vyombo vya ulinzi kumuweka ndani kwa masaa 48 kwa kile alichodai kuwa ali toa lugha ya matusi dhidi yake.
Chanzo: ITV Tanzania
Chanzo: ITV Tanzania

No comments:
Post a Comment