ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 5, 2017

ZIARA YA HAMAD MASAUNI VISIWANI UNGUJA

Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM, NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara Jimboni Welezo, Mkoa wa Mjini Magharibi,Unguja, kufuatilia maeneo sugu yaliyokithiri kwa matendo ya uhalifu ikiwemo utumiaji, uuzaji wa madawa ya kulevya na ubakaji. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Wilaya ya Magharibi A, Unguja, Hamza Khamis Juma. Ziara hiyo imefanyika Visiwani Unguja. Picha na Abubakari Akida.Mbunge wa Jimbo la Welezo, Sada Salum Mkuya akizungumza wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM, NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mhandisi Hamad Masauni(wakwanza kulia), ikiwa na lengo la kukagua maeneo sugu yaliyokithiri kwa matendo ya uhalifu ikiwemo utumiaji, uuzaji wa madawa ya kulevya na ubakaji. Ziara hiyo imefanyika Visiwani Unguja.
Mjumbe wa kamati ya Siasa Jimbo la Welezo,Ayub Saleh, akizungumza wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM, NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia), ikiwa na lengo la kukagua maeneo sugu yaliyokithiri kwa matendo ya uhalifu ikiwemo utumiaji, uuzaji wa madawa ya kulevya na ubakaji.Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Welezo, Sada Salum Mkuya. Ziara hiyo imefanyika Visiwani Unguja.
Mwakilishi Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi,Shawana Buheti, akibadilishana mawazo na Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM, NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mhandisi Hamad Masauni na viongozi wengine akiwemo Mbunge wa Jimbo la Welezo, Sada Salum Mkuya (wakwanza kulia) wakati wa ziara ya Katibu huyo ikiwa na lengo la kukagua maeneo sugu yaliyokithiri kwa matendo ya uhalifu ikiwemo utumiaji, uuzaji wa madawa ya kulevya na ubakaji,Ziara hiyo imefanyika Visiwani Unguja.

No comments: