Na Jumia Travel Tanzania
Ni mara ngapi umeshawahi kusikia ofa mbalimbali za mtangazo ya biashara kupitia vyombo vya habari? Je huwa unashawishika au kuvutiwa nayo mpaka kukupelekea kununua?
Kutoa punguzo la bei ni njia ya haraka zaidi inayotumiwa na wafanyabiashara wengi kuwavutia wateja. Tafiti zinaonyesha umakini wa mteja na ushawishi katika kutumia huduma fulani huja kwa ofa au punguzo la bei. Muda wowote ambao utamwambia mteja kwamba anaweza kuokoa pesa, ipo asilimia kubwa ya kuteka umakini wake na kukusikiliza.
Zipo sababu kadhaa zinazowafanya wafanyabiashara kutoa matangazo ya punguzo katika bidhaa na huduma zao. Sababu hizo zinaweza kuwa kama vile kuwavutia wateja, kuongeza mauzo, kupunguza hifadhi ya bidhaa zisizohitajika dukani, kujijengea jina, kufikia malengo ya kibiashara, na kuokoa gharama nyinginezo za kuendesha biashara.
Tukielekea msimu wa mapumziko ya sikukuu za Pasaka tunaamini utayasikia matangazo ya kila aina yanayokushawishi kutumia huduma fulani. Huduma kama vile za usafiri, mavazi, malazi, samani na kadhalika ni miongoni mwa zitakazokuwa kwenye mzunguko wa vyombo mbalimbali vya habari kukuvutia wewe mteja.
Jumia Travel inaamini kwamba sio watu wote ambao wanatumia ofa hizi ambazo hutangazwa mara nyingi kwenye misimu ya sikukuu kama hii ya Pasaka ambayo inakuja. Inawezekana kukawa na sababu za mtu kuamua kutotumia ofa hizo lakini kuna manufaa mengi tu kama vile:
Kuokoa gharama za matumizi yako ya kawaida. Ni kweli kabisa endapo utakuwa ukifanya manunuzi yako kipindi cha ofa utakuwa unafaulu katika hili. Kipindi pekee ambacho huwa na ofa nyingi ni cha sikukuu na mwisho wa mwaka. Na ni kutokana na uhitaji mkubwa kutoka kwa wateja kwa wakati huo ndio unaowalazimu kufanya manunuzi makubwa.
Lakini pia ofa hurahisisha mahitaji yako kama mteja. Kupitia punguzo la bei unaweza kukuta pesa ambayo ilibidi ununue bidhaa moja unaweza kuongezea na zingine. Hivyo hapo utakuwa umerahisisha mahitaji yako kwa kutumia kiasi kilekile bila ya nyongeza yoyote.
Kwa hali ya maisha ya sasa inabidi mtu kuwa makini sana na namna unavyotumia pesa kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Umakini huo ni pamoja na kufuatilia kwa ukaribu ili kuendana na tabia za wafanyabiashara na soko kwa ujumla.
Fuatilia kujua ni kipindi gani bei za bidhaa na huduma huwa ni za gharama ya juu na ni wakati gani hushuka. Kwa mfano, itakuwa haina maana kununua luninga kwa bei fulani wakati unaweza kuipata kwa nusu bei kipindi cha ofa.
Kwa wafanyabiashara wengi nchini na duniani kote kwa ujumla, hutoa ofa za bidhaa na huduma hasa kipindi cha sikukuu na mwisho wa mwaka. Kwa sababu kipindi hiko uhitaji miongoni mwa wateja huwa ni mkubwa na wako radhi kununua bidhaa au kutumia huduma.
Jaribu kuanza kufuata utaratibu huu kuanzia sasa na uone ni kwa namna gani utakuwa na manufaa kwako. Mwaka bado mbichi, zipo sikukuu kadhaa zinakuja siku za usoni. Jaribu kutembelea Jumia Travel ujionee ofa zilizotolewa na hoteli mbalimbali kwa ajili ya msimu huu wa sikukuu.
No comments:
Post a Comment