ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 19, 2017

Balozi Seif Ali Iddi afanya uzinduzi wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Zanzibar (RSA)

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akionyesha cheti maalum baada ya kuweka saini yake cha kuthibitisha uzinduzi rasmi wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Zanzibar (RSA) hapo Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar. Wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Kamishna wa Kikosi cha Usalama Bara barani Tanzania DCP Mohamed  Mpinga, Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Waziri wa Ujenzi Balozi Ali Karume na Kamishna wa Polisi  Zanzibar (CP) Hamdan Makame.
 Balozi Seif akimkabidhi cheti Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Bibi Narsa Mohamed kutokana  mchango mkubwa uliotolewa na vyombo vya habari vya Shirika hilo wa suala la usalama bara barani.
Balozi Seif akikabidhi cheti maalum kwa Mlezi wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani wa Kanda ya Pwani inayounganisha Tanga na Bagamoyo   Bwana Nurdin Ali kutokana na mchango mkubwa wa Taasisi hiyo uliosaidia kupunguza ajali za vyombo vya moto Bara barani Tanzania Bara. Picha na – OMPR – ZNZ.

Matukio ya uvunjifu wa sheria za usalama Bara barani bado yanaendelea kuoteza nguvu kazi  ya Taifa wakiwemo Vijana wazee na watoto huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu na wengi kuendelea kuwa mayatima katika maisha yao yote.
Akizindua rasmi Mtandao wa Mabalozi wa wa Usalama Bara barani Zanzibar hapo ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi alisema hali hiyo imeendelea pia kuleta hasara kwa Taifa kutokana na kuharibiwa kwa miundombinu  ya Bara bara na vifaa vyengine.
Balozi Seif alisema ajali za bara barani bado zimekuwa ni tishio kwa maisha ya wannchi kutokana na baadhi ya madereva ama kwa makusudi kutotii  sheria na taratibu zilizowekwa katika kufuata matumizi sahihi yaliyowekwa bara barani.
Alisema baadhi ya madereva hao wamekuwa na tabia ya kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo wa kasi bila ya kujali watumiaji wengine  mbali mbali kama watoto ambao nao wana haki ya matumizi ya bara  bara hizo.
Balozi Seif  alionyesha masikitiko yake kutokana na baadhi ya madereva husababisha ajali za kizembe kutokana na ustaarabu wa kisasa ulioingiza wa kuendesha chombo cha moto na huku wanazunguza na simu wakati mataifa mengine Duniani hili wanalihesabu kuwa kosa kubwa bara barani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema uamuzi wa kuanzishwa kwa dhana hii ya mabalozi wa usalama Bara barani  hapa Zanzibar ni wa busara  na kuwa wakati muwafaka ambapo Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada za kukabiliana na ajali za bara barani.
Mapema akitoa Tarifa Mwenyekiti wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani Nd. Justafa Mussa  alisema Mtando huo wa Kiraia umeanzishwa kwa lengo la kulisaidia Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama bara barani kupambana na na makosa yanayotokana na bara bara.
Naye Mlezi wa Mabalozi wa usalama Bara barani Msaidizi Kamishna wa Jeshi la Polisi (ACP ) Mkadam  Khamis Mkadam alisema ajali nyingi zinazotokea  Bara barani kutokana na vitendo visivyotii usalama bara barani.
Alisema ajali za bara barani zilizotokeza mwaka 2016 zilifikia mia 604 na kusababisha vifo vya watu 147 wakati mwaka 2017 uliripotiwa ajali mia 517 zilizosababisha vifo vya watu 133 kukiwa na upungufu wa vifa vya watu 14.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
19/4/2017.

No comments: