ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 11, 2017

Huduma za Benki ya NMB Zasogea Mtaani Kwako

Meneja Uwakala wa Benki ya NMB, James Wanyama (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) walipokuwa wakizinduwa huduma za NMB Wakala zilizoboreshwa zaidi zenye gharama nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za Kibenki wa NMB, George Kivaria. Kwa huduma hizo mteja wa NMB anaweza kuweka na kutoa fedha mtaani kwake, kuangalia salio na hata kufanya malipo ya tozo mbalimbali akiwa katika mawakala wa NMB popote alipo.
Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za Kibenki wa NMB, George Kivaria (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa huduma za NMB Wakala zilizoboreshwa zaidi. Kulia ni Meneja Uwakala wa Benki ya NMB, James Wanyama.

Huduma za Benki ya NMB Zasogea Mtaani Kwako

UPATIKANAJI wa huduma za Benki ya NMB umezidi kuboreshwa na sasa umesogezwa zaidi mtaani kwako. Mteja wa NMB na asiyekuwa mteja kupitia huduma ya NMB Wakala sasa anaweza kuweka kutoa fedha na hata kulipia huduma mbalimbali akiwa mtaani kwake bila ya uhitaji wa kufika katika tawi la benki ya NMB.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari alipokuwa akitambulisha huduma hiyo iliyoboreshwa zaidi, Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za Kibenki wa NMB, George Kivaria alisema kuboreshwa kwa huduma hiyo sasa kunawawezesha wateja kupata huduma za benki hiyo kwa haraka na kwa usalama na uhakika popote walipo.

Alisema huduma hiyo pia inamwezesha mteja wa NMB kuweza kuweka fedha, kutoa, kujua salio lake kwa gharama nafuu zaidi, huku ikitolewa na mawakala zaidi ya 2000 ambao wanapatikana maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo maeneo ya vijijini.

Alisema lengo la NMB ni kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake tena kwa gharama nafuu. Alisema huduma zingine ambazo wateja wengine hata wasiokuwa na akaunti za NMB wanaweza kufanya kwa mawakala hao ni pamoja na kulipa ada za shule, kulipia tozo za luku, ving'amuzi, malipo ya TRA, leseni na bili za maji.

No comments: