ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 26, 2017

KIKOSI KAZI CHA KUNUSURU MTO RUAHA CHATEMBELEA SKIMU YA MWENDAMTITU- MBALARI.

 Mjumbe wa Kikosi  kazi Injinia Seth Luswema (wa kwanza kushoto), akiwa meza kuu pamoja na Viongozi wa Chama kwa wilaya ya Mbalari, Kuanzia kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi, uchumi na maliasili, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Katibu wa CCM wilaya na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mbalari.
 Wajumbe  wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha, wakipata maelekezo  toka kwa Katibu wa skimu ya umwagiliaji ya Mwendomtitu akielekeza juu ya wanavyotumia maji ya umwagiliaji ya Mto Ruaha kumwagilizia mashamba ya mpunga.
 Shamba la vitunguu lililoko karibu na kianziao cha maji cha askimu cha mwendamtitu  wilayani Mbalari likionekana kushamiri  kwa sababu ya maji ya kusukuma na pampu wanayotoa mto Ruaha.
Wajumbe wa Kikosi kazi wakisikiliza maoni ya Wananchi wa kata ya Mwendamtitu walipotembelea skimu yao ya umwagiliaji.

Kikosi cha Kitaifa cha kunusuru Ikolojia ya Mto Ruaha kilichoundwa na Makamu wa Rais wa Tanzania kilichoko Mkoani Mbeya, kimeeendelea na ziara yake kwa kutembelea skimu ya Mwendamtitu iliyopo wilayani Mbarali. Katika ziara hiyo Kikosi kazi kiligundua jinsi ambavyo miundombinu ya skimu hiyo inavyopoteza maji ambayo yalitakiwa kuingia Mto Ruaha. Aidha pia kimegundua kuwa skimu hiyo imeanzishwa pasipo kufuata sheria za umwagiliaji kwani haina kibali cha umwagiliaji wala kibali cha matumizi ya maji yanayoingia katika mfereji wa skimu hiyo.
Wakiongea katika ziara hiyo Wajumbe wamesikitishwa na kitendo cha skimu hiyo cha kutumia maji mengi pasipo kuwa na kibali chochote wala pasipo kuwa na miundombinu ya mifereji inayowezesha maji kurudi mto Ruaha mKuu." Katika skimu hii  Maji yanatitririka bure na kwa aina hii ya umwagiliaji kamwe mto Ruaha Mkuu hautapata maji, ila tutachukua hatua stahiki" aliongea Mjumbe   Injinia Seth Luswema.
Kwa upande wa wananchi wa eneo hilo wameiomba Serikali iwasaidie kuwapatia elimu jinsi ya kuendesha skimu hiyo na pia kuelekezwa jinsi ya kuweka miundombinu rafiki kwa ajili ya kuokoa kiasi cha maji kinachopotea. Wamesema wao hawana elimu yoyote na hawajui kama wanakosea kwa jinsi wanavyoendesha skimu hiyo.
Kikosi hiko bado kipo Mkoani Mbeya katika wilaya ya Mbalari kwa ajili y akuzungukia na kukagua maeneo mbalimbali amabayo yanachangia maji kutokwenda Mto Ruaha Mkuu.

No comments: