Mfereji wa kutolea maji kupeleka mto Ruaha Mkuu ulioko ndani ya Shamba la Mpunga la Kapunga ukiwa umejengewa tuta ili kutopitisha maji hayo kuelkea mto Ruaha kama inavyotakiwa.
Magugu na nyasi zikionekana katika mfereji wa kupitishia maji katika shamba la Mbarali ambapo magugu hayo huzuia maji kutopita kwa urahisi.
Mwenyekiti wa kikosi kazi cha Kitaiafa cha kunusuru ikolojia
ya Mto Ruaha Bwana Ricahrd Muyungi
akitoa maelekezo na maagizo kwa Wamiliki wa mashamba ya mpunga ya Highland
Estates juu ya wanachotakiwa kufanya baada ya shamba alo kukutwa chafu sana na
mifereji yao yote imejaa magugu maji.
Kampuni inayojishughukisha na kilimo cha Mpunga ijulikanayo kwa jina la Highland Estates iliyopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya imepewa agizo na Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha kilichoko mkoa wa Mbeya kuwa ndani ya mwezi mmoja wahakikikishe wamesafisha mifereji yote inayozunguka ndani ya shamba lao kwa kujenga upya miundombinu inayopoteza maji , kung'oa magugu maji na nyasi zote zilizoota katika mifereji ya matoleo ya maji ndani ya shamba hilo kwani inazuia maji kupita kwa urahisi kuelekea Mto ruaha kama inavyotakiwa. Pia wametakiwa kuanza taratibu za kupatiwa cheti cha ukaguzi wa athari za mazingira kitoka Baraza lau Usimamizi wa mazingira (NEMC).
Akiongea katika ziara hiyo Mwenyekiti wa kikosi kazi hiko Bwana Richard Muyungi alisema Uongozi wa shamba hilo wafanye juhudi za ziada kutunza mazingira yote yanayozunguka shamba hilo na kuhakikisha maji yanapita kwa urahisi katika mifereji ya matoleo ya kupeleka maji mto Ruaha Mkuu. "Tunawapa mwezi mmoja mfanye ukarabati na mrekebishe hali ya usafi katika mifereji ya shamba lenu baada ya muda huo tutarudi kwa ajili ya kukagua." Alisema Muyungi
Kikosi kazi hiko pia kilitembelea katika shamba la Mwekezaji lililopo wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya lijulikanalo kama Kapunga Rice Project. Kikosi kiliona matumizi mabaya ya maji kwa kuyachepusha bila vibali kunakofanywa na Wananchi walio maeneo ya jirani. Badala ya mifereji ya maji iliyopo shambani hapo kurudisha maji mto Ruaha Mkuu. Maeneo mengi ya mifereji ya kutolea maji katika shamba hilo na kupeleka mtoni yamezibwa kwa viroba na udongo ili maji yasiende mto Ruaha. Kikosi kazi kilielekeza Kamuni michepusho yote ya maji ifungwe mara moja na Kampuni isimamie na kugharamia shughuli hiyo. Maagizo hayo yote yametakiwa kukamilika mpaka siku ya jumanne ya tarehe 25 Aprili 2017.
Kikosi kazi hiko cha Kitaifa kilichopo Mkoani Mbeya bado kipo katika ziara ya kutembelea sehemu mbalimbali ili kujua, kufahamu, kuona na kupata maoni mbalimbali ya Wananchi ni nini haswa kinachosababisha maji kutokuingia katika mto Ruaha ili kutoa suluhisho la kudumu.
No comments:
Post a Comment