Advertisements

Saturday, April 22, 2017

POLISI WAUA WATATU WANAODHANIWA KUWA MAJAMBAZI

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Pwani. Utata umezuka baada ya kuwepo kwa taarifa za polisi kuua watu sita wanaodaiwa kuwa majambazi wilayani Kibiti.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga alisema anafuatilia ukweli wa tukio hilo.

Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Nsatu Marijani, alisema kama taarifa hizo zingekuwa za ukweli basi jeshi hilo lingetoa taarifa.

Hata hivyo, chanzo kimoja cha habari kutoka wilayani humo kililiambia Mwananchi kuwa polisi imewaua watu sita.

Pia chanzo hicho kilieleza kuwa milio ya mabomu na risasi ilisikika katika maeneo kadhaa ya kijiji cha Jaribu , Mpakani, wilayani humo.

Tutaendelea kukujuza kuhusu taarifa hii.

No comments: