ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 23, 2017

Ushindi wa Serengeti Boys wapa jeuri kocha

By Eliya Solomon, Mwananchi

Dar es Salaam. Serengeti Boys imeendelea kujimalisha kuelekea katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, baada ya kuitandika Gabon kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Morocco.

Katika mchezo huo mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Kelvin Naftali na Ibrahim Abdallah na kujihakikishi ushindi huo muhimu jijini Rabat ikiwa kambini ijiandaa na fainali za zitakazoanza Mei 14 -28 nchini Gabon.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema vijana wake walicheza vizuri japo kuna makosa madogo madogo wameyabaini kwenye kikosi hicho.

"Nilisema tutatafuta matokeo ya ushindi na kuhusu hilo tumefanikiwa, kikosi kinaendelea kujengeka kwenye hali ya kujiamini kutokana na matokeo ambayo tumekuwa tukiyapata.

"Kimsingi ni vizuri kumshukuru Mungu kwa kila hatua naamini tumefikia katika hatua ya kutia moyo kuelekea katika mashindano.

Naye mfungaji wa bao la kwanza kwa Serengeti Boys, Naftali alisema ushindi walioupata ni mwendelezo mzuri wa maandalizi yao.

"Kushinda kwetu kunaongeza hali ya kujiamini katika michezo yetu ya mbele toufati na tukifungwa na ukiangalia timu tunazocheza nazo zipo kwenye mashindano" alisema mchezaji huyo.

Serengeti Boys watacheza tena na Gabon Jumanne kabla ya kwenda Cameroon watakapo weka kambi ya wiki moja pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na wenyeji wao.

No comments: