Wakazi wa tarafa ya Wangingo’mbe mkoani Njombe wako hataraini kukumbwa na baa la njaa kutokana na eneo la tarafa hiyo mvua kukatika kabla ya mazao yao kukomaa kutokana na uharibifu wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji.
Akizungumza mbele ya kikosi kazi kilichoundwa na Makamu wa raisi Samia Suluhu Hassani kwaajili ya kuitunza ikojia ya Mto Ruaha Afisa kilimo wa wilaya hiyo Bernadeta Fivao amesema kuwa licha ya serikali kuzuia wananchi kulima kwenye vyanzo vya maji kunawezekano mkubwa kwa wakulima wa tarafa hiyo kundelea kulima kwenye vyanzo vya maji kutokana na kukosa chakula.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya wangingombe wamekiambia kikosi kuwa wanasiasa wakiwemo madiwani na wabunge wamekuwa wakihamasisha wananchi kuendelea kuharibu vyanzo vya maji.
Eneo la tarafa ya Wangingombe limekuwa likikabiliwa na tatizo la uhaba wa maji kutokana na ufugaji holela pamoja uharibifu wa vyanzo kwa kufanya kilimo cha mazao kando ya vyanzo vya maji na mito maarufu kama Vinyungu.
No comments:
Post a Comment