NA
K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
WATANZANIA
wanane waliokuwa kizuizini nchini Malawi wakituhumiwa kufanya “ushushushu”
wameachiliwa huru leo Aprili 13, 2017 na mahaka moja kwenye mji wa Mzuzu nchini
humo.
Taarifa
za vyombo vya habari vya Malawi zinasema, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya
Muzuzi nchini Malawi, amewaachia huru Watanzania hao waliotiwa mbaroni Desemba
20, 2016 kwa tuhuma za kufanya “ushushushu” kwenye mgodi wa madini ya Urani wa
Kayekera huko Karonga.
Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari, Watanzania
hao walikuwa wakishtakiwa kwa kosa la kuingia maeneo ya mgodi bila kibali ikiwa
ni pamoja na shkata la kufanya “upelelezi”.
Hata
hivyo Watanzania hao walikanusha mashtaka hayo tangu walipotiwa mbaroni.
Kwa
mujibu wa Watanzania hao, sababu kuu iliyowafanya kufika kwenye eneo hilo
ilikuwa ni ziara ya kimafunzo na wala haikuwa kufanya upelelezi kama ambavyo
mamlaka za Malawi zilivyowatuhumu.
Baada
ya Watanzania hao kupatikana na hatia, Hakimu huyo Mkuu Mkazi wa mahakama ya
Muzuzu, Texious Masoamphambe, aliwahukumu Watanzania hao kifungo cha mwezi
mmoja jela kwa kosa la kuingia eneo hilo bila kibali na kifu ngo cha miezi
mitatu jela kwa kosa la kufanya “Ushushushu”
Hata
hivyo Hakimu huyo aliitupilia mbali hukumu hiyo na kutoa sharti la watu hao
kutofanya kosa katika kipindi cha miezi sita.
Pia
mahakama hiyo iliiamuru serikali kuwafukuza nchini Watanzania hao.
Aidha kuachiwa huru kwa Watanzania hao ambao tayari walikuwa wamekwisha hukumiwa kunatokana na mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea baina ya Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, ambapo Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt.Augustine Mahiga, alinukuliwa wiki iliyopita akitoa hakikisho la kuachiwa huru kwa Watanzania hao.
No comments:
Post a Comment