Mmiliki wa shule ya Lucky Vicent Arusha Innocent Moshi na Makamu Mkuu wa shule Longino Vicent Nkana jana wamefikishwa Mahakamani na kusomewa makosa matano.
Mwendesha mashtaka wa Serikali Rose Sule alisema mnamo May 6 Mmiliki huyo wa shule aliruhusu Dereva kuendesha gari la abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji, kutumia gari bila kuwa na BIMA pamoja na kushindwa kuingia mkataba na Mwajiriwa.
Watuhumiwa wote waliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuwa na watu wawili kwa bondi ya milioni 15 kila mmoja na huku washtakiwa kutoruhusiwa kuondoka ndani ya mkoa ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hati zao zakusafiria.
Hakimu wa Mahakama ya hakimu mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Desdery Kamugisha aliahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 8 mwezi wa 6 kutokana na upelelezi kutokamilika.
No comments:
Post a Comment