Advertisements

Friday, May 19, 2017

Upasuaji majeruhi wa Lucky Vincent wafanikiwa Marekani


Doren Mshana 

HALI za wanafunzi majeruhi wa shule ya Lucy Vincent ya mkoani Arusha, waliopelekwa hospitali ya Mercy jijini Sioux katika jimbo la IOWA nchini Marekani kwa matibabu inaendelea vizuri na tayari wote watatu wamefanyiwa upasuaji.

Majeruhi Sadya Awadh na Wilson Tarimo wote walifanyiwa upasuaji jana wakati Doren Mshana alifanyiwa juzi. Mtu wa Karibu anayefuatilia afya za watoto hao na Mbunge wa Singida Kaskazini na rafiki wa karibu wa watalii madaktari waliowaokoa majeruhi na kuopoa maiti siku ya ajali Mei 6, mwaka huu.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la kilima cha Rhotia, Karatu na kusababisha vifo wanafunzi 32 wakiwemo walimu wawili wanafunzi na dereva, aliandika hayo katika ukurasa wake wa Facebook jana.

Nyalandu alisema: “Kila mtoto amewekwa kwenye chumba chake peke yake, na mama mzazi na muuguzi mmoja wanakuwa naye wakati wote.” Mbunge huyo alisema Sadya amefanyiwa upasuaji maeneo matatu yaliovunjika ikiwemo mkono wa kulia lakini shingo haikufanyiwa upasuaji na badala yake aliwekewa kifaa cha kunyoosha (Brace) atakayokaa nayo wiki sita kuanzia sasa.

“Wote wanaendelea na mapumziko katika hospitali ya Mercy, Sioux City. Mungu ni mwema sana,” aliandika Nyalandu. Katika hatua nyingine, kutokana na ajali hiyo, Polisi wa mkoani humo limetangaza kiama kwa kuyakamata magari yote mabovu yasiyokidhi viwango vya kusafirisha wanafunzi yanayotumiwa na wamiliki wa shule za watu binafsi Jijini hapa.


Akizungumza na wamiliki wa shule binafsi mkoani hapa, Mkuu wa polisi wa usalama barabarani Mkoani Arusha, Nuru Seleman alisema kuwa kuanzia sasa polisi kupitia askari wake wa usalama barabarani halitasita kuchukua hatua kwa magari ya kusafirisha wanafunzi ambayo hayatakuwa katika ubora unaotakiwa na yakizidisha idadi ya wanafunzi na yasiyokuwa na kibali cha usafirishaji wa abiria yatakamatwa.

Aliwaonya wamiliki wa shule kutoruhusu magari ya namna hiyo kutokuwepo barabarani kupakia wanafunzi kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria za usalama barabarani na watachukuliwa hatua kali.

Aidha aliwataka wamiliki wa shule hizo kuwaajiri madereva hao na kuwapatia mikataba inayotambuliwa na serikali sambamba na kuwapa mafuzo maalumu ya kubeba wanafunzi

HABARI LEO

No comments: