Advertisements

Wednesday, May 17, 2017

PICHA MNADA WA HARAMBEE KUCHANGIA WATOTO YATIMA ST. EDWARD CHURCH BALTIMORE

BARUA YA SHUKURANI

Waumini Wakatoliki (DMV) pamoja na Fr. Honest Munishi tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mheshimiwa Baba Askofu wa Jimbo Kuu la Tabora Askofu Mkuu Paul Ruzoka kwa kusalisha Misa ya Jumapili, Balozi Liberata Mulamula Mgeni wetu rasmi na Wana DMV wote walioshiriki nasi katika misa ya kusherehekea siku ya Wakina mama Duniani iliyofanyika Jumapili tarehe 14 Mei, 2017 katika Kanisa Katoliki la Mt. Edwards lililopo Baltimore, Maryland pamoja na harambee ya kuchangia watoto yatima nyumbani Tanzania. Michango yenu itakuwa chanzo kikubwa cha kuwasaidia watoto hao na fedha zilizopatikana jana kwenye michango ya watu binafsi, Mch. John Mbatta, makampuni ya Watanzania yafuatayo:- Alpha Home Care, B and B Transportation, Eddah’s Elegant Catering, Global Style llc, JB Auto and Tires, Julia Shirima Co., Karibu Grill, Mega Tires, Metro Tires llc, Praise Home Care Services, Sagun Home Care Inc., TAHECO na TAMCO zitapelekwa katika Kituo cha watoto (ALBINO) Jimbo la Tabora kilicho chini ya Askofu Mkuu Paul Ruzoka.

Ahsanteni sana! Mwenyezi Mungu awabariki na awazidishie maradufu pale mlipotoa.

Kwa niaba ya Jumuiya ya wakina mama wakatoliki, Wakatoliki DMV na Fr. Honest Munishi ni mimi Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wakatoliki DMV,

Patrick Kajale.

Patrick .M.Kajale
1417 Crockett Lane
Silver Spring,MD 20904.
Cell # : 301-755-7836

Dada Joyce akitoa maelezo Kwa niaba ya kina mama Wakatoliki kwa mgeni rasmi Balozi Mulamula kabla ya kuanza rasmi kwa harambee.
Baba Askofu mkuu wa Jimbo la kuu Tabora Paul Ruzoka na mgeni rasmi Balozi Mulamula wakikata utepe kuzindua harambee yakuchamgia watoto.
Meza kuu ikiongozwa na Baba Askofu mkuu Paul Ruzoka mwenye kofia, Balozi Mulamula, Fr. Munishi na watawa wengine kutoka Washington DC.
Meza kuu ikiongozwa na Baba Askofu mkuu Paul Ruzoka mwenye kofia, Balozi Mulamula, Fr. Munishi, kanali Mutta na mama Mutta na watawa wengine kutoka Washington DC.
Masista kutoka majimbo mbali mbali kutoka Marekani wakiwa pamoja na waumini wengine.
Kamati maalumu ya umoja wa kina mama Wakatoliki iliyoandaa na kufanikisha harambee hii ikiongozwa na Makamu wa mwenyekiti Thecla Kessy wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Fr. Munishi na wageni waalikwa kutoka jumuiya ya kiislamu DMV (TAMCO).

Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Masista kutoka majimbo mbali mbali kutoka Marekani wakiwa pamoja na waumini wengine.
Meza kuu wakifuatilia kwa karibu harambee ya kuchangia watoto yatima
Wageni waalikwa kutoka Chama cha waisilamu DMV(TAMCO)Asha, Joha Nyanganyi na Asha wakiwa na wanajumuiya ya Wakatoliki.
Meza ya vinywaji ikiongozwa na kaka Damas na Kimolo
Meza ya vinywaji ikiongozwa na kaka Damas na Kimolo

No comments: