Serikali imefurahishwa na na juhudi za Mfuko wa Pensheni PPF kwa kutoa
msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 99,983,700 kwa hospitali
16 hapa nchini ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha
sekta ya afya hapa nchini.
Akielezea furaha hiyo wakati akipokea
sehemu ya msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6 kwa
hospitali ya mkoa wa Morogoro, Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Zainab Chaula amesema kumekua na
chanagamoto mbalimbali za vifaa tiba katika hospitali mbalimbali hapa
nchini.
Kwa upande wake meneja wa uhusiano wa PPF, Lulu
Mengele amesema pamoja na kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine
yanayoendana na hayo kwa wanachama wake kutoka kwenye sekta rasmi na
isiyokuwa rasmi. Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sera yake ya uchangiaji
na udhamini ambapo moja kati ya sehemu wanayochangia ni upande wa sekta
ya afya ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi
milioni 99,983,700 zimetolewa kununulia vifaa tiba vinavyogawiwa katika
hospitali na vituo vya afya 16 vya serikali nchini. Sehemu ya vifaa
hivyo vilivyotolewa ni muendelezo wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba
lilizinduliwa na waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa 26 wa wanachama na wadau
wa PPF uliofanyika machi 2017 jijini Arusha.
Naye meneja wa PPF
kanda ya mashariki na kati, Bw. Michael Christian alisema kuwa PPF wanao
mfumo wa uchangiaji wa hiari 'WOTE SCHEME' ambapo aliwakaribisha
wananchi waliokatika sekta isiyo rasmi kujiunga ili kunufaika na mafao
ya uzeeni, huduma za bima za afya pamoja na mikopo ya elimu na mikopo ya
maendeleo. Vile vile wale walio sekta rasmi wanakaribishwa kujiunga
kama mfumo wa hiari ili kuweza kujiwekea akiba na kunufaika na mikopo ya
elimu na mikopo ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment