Shirika la Afya Duniania (WHO)
limetangaza kuwapo kwa mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola katika
nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mtu apataye mmoja amefariki baada ya
kupata virusi vya Ebola kaskazini mashariki mwa DRC kwa mujibu wa
WHO.
Wizara ya Afya ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo imeifahamisha WHO kupitia twitta vipimo vya
maabara vimebaini mtu huyo alikuwa na virusi vya Ebola.
Zaidi ya watu 11,000 walifariki
dunia kwa ugonjwa Ebola katika mataifa ya Afrika Magharibi mwaka
2014-2015, wengi wakiwa wa nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia.
No comments:
Post a Comment