ANGALIA LIVE NEWS
Saturday, May 6, 2017
WANAFUNZI 33 NA WALIMU WAO WATATU WAFARIKI KATIKA AJALI ARUSHA
NA K-VIS BLOG, ARUSHA
WATU 37 wakiwemo wanafunzi 33 wamefariki dunia katika ajali ya basi wilayani Karatu leo Mei 6, 2017.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema, ajali hiyo pia imeua walimu watatu na dereva wa basi hilo mali ya shule ya msingi ya LuckyVincent Nursery and Primary School ya Kwa-Mrombo jijini Arusha.
Katika ajali hiyo iliyotokea baada ya basi hilo kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo la mto Malera kandokando ya barabara kuu ya Karatu, kata ya Rhotia wilayani humo, imeelezwa kuwa wanafunzi hao ni wa darasa la saba na walikuwa wakieleeka Karatu kufanya mtihani wa ujirani wmema na wenzao wa shule ya msingi Tumaini iliyoko wilayani humo.Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutoka kwa ajali hiyo mbaya.
Munguazilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amin.
Waziri Mkuu wa zamani, na mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mhe. Edward Lowassa katika salamu zake za rambirambi zilizotumwa mapema leo amesema“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za ajali mbvaya sana iliyotokea leo asubuhi wilayani karatu, wanafunzi kadhaa na walimu wao wamepoteza maisha, ni ajali mbaya iliyoifanya siku hii iwe siku mbaya sana ktika historia ya nchi yetu, nawapa pole wote waliopatwa na maafa haya nawataka watanzania tusimame pamoja kusaidiana kwa jambo lolote tutakalopaswa kufanya wakati huu mgumu”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment