Advertisements

Saturday, May 6, 2017

MVUA ZACHUKUA MAISHA YA MAMA NA MWANA TANGA

By Burhani Yakub.Mwananchi.; byakub@mwananchi.co.tz.

Korogwe. Mwanamke mmoja Happiness Mvita (24) pamoja na mwanaye Prisca Lugi (4) wamekufa kwa kusombwa na maji huku wengine wanane wakijeruhiwa kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba amesema tukio hilo limetokea jana asubuhi katika kijiji cha Magila Kata ya Mkumbara Wilayani hapa.

Aliwataja waliokufa kwa kusombwa na maji kuwa ni Happiness Mvita (24) na mwanaye Prisca Lugi (4) huku wengine wanane wakijeruhiwa kwa matukio tmbalimbali ya kuangukiwa na kuta.

Alisema miongoni kwa waliojeruhiwa yupo mtoto wa umri wa chini ya mwaka mmoja na kwamba majina yao yatatolewa baadaye.

"Majeruhi wapo katika hospitali ya Wilaya ya Korogwe ya Magunga kwa matibabu." alisema

Kamanda Wakulyamba na kuwataka wananchi kuwa waangalifu kipindi hiki cha mvua.

Mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini,Stephen Ngonyani (Profesa maji Marefu ametuma salamu za rambirambi kwa wafiwa na majeruhi.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu alisema waliokufa pamoja na majeruhi ni wapiga kura wake hivyo ataungàna nao katika mazishi na kufuatilia matibabu kwa waliolazwa.

No comments: