Figure 1Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig Jen. (mst.) Emmanuel Maganga akihutubia washiriki wa Mafunzo ya PPD katika Ukumbi wa Hoteli ya Lake Tanganyika
aliongeza kuwa kuna sababu nyingi za kifursa Mkoani Kigoma ikiwemo hali ya hewa nzuri, jiografia yenye fursa, madini, utalii, ardhi yenye rutuba na Ziwa Tanganyika. Hizi ni fursa kubwa katika biashara zikitumiwa ipasavyo uchumi wa Mkoa wa Kigoma utapaa.
Ameziagiza Halmashauri zitengeneze mipango mikakati ya namna ya kuweka miundombnu mizuri ya kibiashara ikiwemo kutenga maeneo ya uwekezaji. Alisema nchi yeyote haiendelei kwa kuwa na rasilimali tu bali uwepo wa mipango mathubuti na wataalam wanaoweza kushauri namna bora ya kutumia rasilimali hizo. Tuchangamkie furasa hii, kwa kunadi fursa zilizopo Mkoani Kigoma.
Figure 2 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Hussein Juma Ruhava akikabidhiwa Cheti cha Ushiriki wa Mafunzo kati Sekta binafsi na sekta ya Umma katika uboreshaji Mazingira ya Biashara Mkoani Kigoma
Ametoa wito kwa mashirika mbalimbali na Taasisi binafsi kuanziasha viwanda vidogovidogo ambavyo havihitaji gharama. Aidha amewataka wafanyabiashara wafanye biashara halali na kuzingatia sheria za nchi hasa ulipaji wa kodi.
Mafunzo hayo yalifanyika chini ya ufadhili wa TCCI, BEST, na LIC kwa lengo la kujadili na kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya biashara Mkoani Kigoma na namna ya kushirikiana kati ya sekta binafsi na sekta ya umma kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia wawekezaji.
Mashirika yasaidia Sekta ya Afya Mkoani Kigoma
Sekta ya Afya Mkoani Kigoma imeimarika kutokana na Mashirika ya Thamini Uhai, Bloomberg Foundation na Engeder Health kujikita katika kusaidia Mkoa katika sekta ya Afya.
Figure 3 Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Tathmini ya Sekta ya Afya huduma ya Mama na Mtoto Mkoani Kigoma
Mashirika hayo yasiyo ya kiserikali yanatarajiwa kukabidhi miradi ikiwemo Miundombinu ya Majengo ya maabara, vifaa tiba, kugharimia posho za watumishi wa Afya wanaojitolea katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kigoma hasa pembezoni.
Wakiongea kwa nyakati tofauti tofati wawkiishi wa mashirika hayo wameuomba Uongozi wa Mkoa kujiandaa kupokea miradi hiyo na kuitunza pamoja na kuiendeleza kwa manufaa ya wananchi wa Kigoma.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ameyapongeza mashirika hayo kwa kuwa na moyo wa dhati katika kuwasaidia wananchi wa Mkoa wa Kigoma katika masuala ya Afya, aidha aliongeza kuwa sekta ya Afya Mkoa wa Kigoma imeimarika, zaidi Mkoani Kigoma kutokana na Serikali kushirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali na alisema kwa sasa Mkoa unatarajia wafayakazi wengi zaidi kuletwa Mkoani Kigoma kama ilivyo adhma ya Serikali ya awamu ya Tano.
No comments:
Post a Comment