Advertisements

Friday, June 23, 2017

SBL YAZINDUA MRADI WA MAJI KWA WAKAZI WA CHANG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia) pamoja na Meneja Uwajibikaji wa SBL, Hawa Ladha (kulia) wakimtwika ndoo ya maji mmoja wa kinamaa leo ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia) pamoja na Diwani Kata ya Chang'ombe, Benjamin Ndalichako (kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Temeke, Primy Damas (katikati) akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo mara baada ya kuzinduliwa. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie na Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Benjamin Ndalichako wakishuhudia.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.

KAMPUNI ya Bia Serengeti leo imezindua mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada za kuwaletea maji safi na salama wakazi wa eneo hilo.
Ukiwa na uwezo kwa kuhudumia watu 4,000 mradi huo unajumuisha kisima pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji ambapo zinazalishwa lita 20,000 za maji kwa kila masaa ishirini na nne.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Helene Weesie alisema kuwa mradi huo ambao unajulikana, “Maji kwa Uhai” ni miongoni mwa mikakati kama hiyo ambayo kampuni ya bia imeiendesha katika mikoa ya Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwa inawanufaisha zaidi ya watu milioni moja kwa maji safi na salama.
Weesie alisema kwamba mradi wa Chang’ombe sio tu kwamba utaboresha afya za wakazi wa eneo hilo bali pia utaongeza tija kiuchumi, “hususani kwa watoto wa kike na wanawake ambao hawatahitaji kutumia saa nyingi kutafuta maji safi sehemu nyingine. Hii inawapa fursa ya kuhudhuria shule wakiwa huru.”
“SBL ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu na Maji kwa Uhai ikiwa ni mojawapo ya maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeyabainisha katika lengo lake kuipatia jamii msaada katika jumuia inamohudumia”, alisema Weesie akielezea vipaumbele vingine hivyo kama: Kutoa Stadi za Maisha, Undelevu wa mazingira na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.
Mkurugenzi huyo Mtedaji aliendelea kusema SBL ina programu ya kilimo ambayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imewasaidia wakulima zaidi ya 100 nchini kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha iliyowasaaidia kuboresha maisha yao na maisha ya jumuia zao.
Weesie alisema kutokana na juhudi hizo, “SBL imeweza kuibua tani za malighafi inazotumia kutoka wa wakulima wa hapa nchini kutoka 0 hadi tani 10,000 na hili limechangia katika kukua kwa kampuni na kukuza kipato cha wakulima.”
Aliendelea kubainisha: “Licha ya kuchangia katika kukua kwa uchumi wa taifa kupitia malipo ya kodi ya mara kwa mara, SBL imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa hususani katika kutoa huduma ya maji safi na salama ndani ya nchi.”
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia) pamoja na Diwani Kata ya Chang'ombe, Benjamin Ndalichako (kushoto) wakisfurahia mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji.
Muonekano wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva aliipongeza SBL kwa kutoa msaada uliokuwa unahitajika mno, akisema kwamba kampuni hiyo ya bia imekuwa mstari wa mbele katika kukuza miradi ya maendeleo nchini ambayo inawezesha kuwepo kwa jamii inayozalisha na iliyo na afya.

No comments: