ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 31, 2017

BALOZI WA KUWAIT ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI JIJINI DAR ES SALAAM

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimkabidhi zawadi Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (kushoto), baada ya mazungumzo na Balozi huyo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (Wakwanza kulia) alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem, akizungumza wakati wa kikao na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (katikati) na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akiongozana na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (kulia) alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo kwa mazungumzo yaliyohusisha ushirikiano kati ya Majeshi ya nchi hizo kubadilishana Utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo kwa mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye(hayupo pichani). Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (katikati) baada ya kikao cha mazungumzo yaliyohusisha ushirikiano kati ya Majeshi ya nchi hizo katika kubadilishana Utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji


Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, liko katika mkakati wa kuingia ushirikiano na Serikali ya Kuwait katika shughuli zake za kukabiliana na majanga ya moto ikiwa ni juhudi zake katika kuyafikia maeneo mengi nchini. 

Akizungumza alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es salaam, Balozi wa Kuwait Nchini, Jasem Al-Najem, alisema serikali ya Kuwait ipo tayari kubadilishana mafunzo na kutoa msaada wa vifaa kwa Jeshi hilo.

“Ni vema tukatengeneza mpango ambao wataalam wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka nchini Tanzania wataweza kubadilishana uzoefu na wataalamu kutoka nchini Kuwait kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na majanga pindi yanapotokea, ’’ Alisema Balozi huyo.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye alimshukuru kwa kumtembelea na kusema kuwa ujio wa balozi huyo, umefungua ukurasa mpya kwa upande wa misaada na mafunzo kwa Askari wa Jeshi hilo, kwani watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuongeza tija kwa Jeshi lake.

“Tutapata nafasi ya kubadilishana uzoefu na kupata mafunzo kutoka Nchi ya Kuwait na kuongeza ufanisi katika majukumu yetu ya kila siku, lengo ikiwa ni kukabiliana na majanga mbalimbali yakiwemo ya moto,’’ alisema Kamishna Jenerali.

Katika kikao hicho Balozi wa Kuwait, Nasem Al-Najem alipokea taarifa ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo ikiwemo uhaba wa vitendea kazi huku akiahidi kuzifanyia kazi na akisisitiza mchakato wa kusaini makubaliano ya hiari ukamilike kwani utakuwa msaada wa kutekeleza kwa haraka program za mafunzo ya muda mfupi.


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

No comments: