Advertisements

Thursday, July 20, 2017

LOWASSA AWASILI TENA POLISI KUHOJIWA

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amewasili leo, Julai 20 saa mbili asubuhi makao makuu ya Jeshi la Polisi kwenye ofisi za Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Lowassa ameambatana na mkewe, Regina na mwanasheria wake, Peter Kibatala.

Hii ni mara ya nne kwa Lowassa kuripoti hapo akituhumiwa kutoa kauli za kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa  Juni 23, na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa gerezani  akidai utaratibu wa kisheria ufanyike ili waachiwe huru.

Polisi wameimarisha ulinzi eneo hilo, huku Lowassa akiwa ndani tayari kwa kuhojiwa.

No comments: