Mbunge wa Ilala ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge Mhe Mussa Azzan Zungu akiongoza kikao baina ya Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kikao baina ya Makamishina hao ambacho lengo kubwa lilikuwa ni kubadilishana uzoefu wa utedaji kazi kiliongozwa na Mhe Zungu kwa niaba ya Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania. Makamishina hao wa Bunge la Uganda wapo nchini kwa ziara ya Kibunge ya siku mbili.
Kiongozi wa Msafara Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda Mhe Cecilia Ogwal (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa kikao baina ya Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge mbaye pia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania Dkt. Thomas Kashililah akizungumza wakati wa kikao baina ya Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania (waliokaa) na baadhi ya Watumishi wa pande zote mbili katika picha ya pamoja mara baada ya kikao.
(Picha na Ofisi ya Bunge)
No comments:
Post a Comment