ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 12, 2017

MAREHEMU SETH KATENDE AAGWA NA KUZIKWA KWENYE MAKABURI YA KINONDONI LEO

MWILI wa marehemu Seth Katende ‘Bikira wa Kisukuma’, aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Efm, kipindi cha Ubaoni, umeagwa katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya kumalizika kwa shughuli hizo, safari ya kuelekea kwenye makazi yake ya milele, kwenye Makaburi ya Kinondoni ilianza ambapo hatimaye maziko yamefanyika mchana wa Juni 12, 2017.
Bikira wa Kisukuma, alifariki juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwa mujibu wa baadhi ya wafanyakazi wenzake ambao hawakutaka kutajwa majina yao kwa vile siyo wasemaji, walisema marehemu alianza kuugua kiasi cha mwezi mmoja uliopita na msiba uko nyumbani kwa baba yake mzazi huko Changanyikeni.
Marehemu ambaye alikuwa akitangaza kipindi cha Ubaoni, kinachorushwa na redio hiyo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, saa kumi jioni, alikuwa pia ni bloga maarufu katika mitandao ya kijamii
 MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akitoa salamu zake wakati wa kuagwa kwa mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akitoa salamu zake kwa famila, ndugu na jamaa.


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitoa salamu zake wakati wa kusaliwa na kuagwa kwa mwili wa  mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni, likiwa katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Baba wa marehemu, Mzee Katende (wa kwanza kushoto) akiwa ndugu zake marehemu wakiaga mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar.
Mke pamoja na mtoto wa marehemu wakiaga mwili 
 MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiaga mwili mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar
 Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob akiaga mwili mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma  leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiaga mwili mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akiaga mwili mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar
Mkurugenzi na mzalishaji wa vipindi waClouds Media Group, Ruge Mutahaba(mwenye shati nyeusi) akiaga mwili mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar
Mtangazaji waClouds FM Gardner G Habash akiaga mwili

Mtangazaji wa EFM, Mpoki 'Mwarabu wa Dubai'( katikati) akiwa ameshikiriwa mara baada ya kuanga mwili wa Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar

  

 

  Sehemu ya Waombolezaji wakiwa katika Viwanja Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam kunakofanyika misa ya kuaga mwili wake hivi sasa, ambapo baada ya kumalizika kwa misa hiyo, Mwili wa Marehemu utapumzishwa kwenye nyumba yake ya Milele katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam mchana wa leo.
 

 
 Baba wa marehemu, Mzee Katende akiwa ameshikiliwa mara baada ya kuaga mwili wa kwanae Marehemu Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma   leo kwenye viwanja vya Leaders leo jijini Dar 


  



1 comment:

Lee said...

Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi Amen