ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 12, 2017

Tucta wamuangukia Magufuli kwenye vyeti feki

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) wamemuomba Rais John Magufuli kuangalia upya watumishi waliokutwa na vyeti feki ambao wamebakisha mwaka mmoja kustaafu waweze kulipwa mafao yao.
Itakumbukwa hivi karibuni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa hakuna mafao kwa waliobainika kutumia vyeti feki.
Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya amesema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari.
Nyamhokya alimpongeza Rais kwa kusimamia vizuri zoezi hilo hivyo wanamuomba kuwafikiria watumishi waliobakiza mwaka mmoja kustaafu walipwe mafao yao ili kukabiliana na ugumu wa maisha waliokuwa nayo.
"Kuna watumishi waliingia kwa magendo bila ya Serikali kujua matokeo yake wamefukuzwa kwa kuwa na vyeti feki huku wakibakisha mwaka mmoja kustaafu, hivyo tunaomba Serikali iwafikirie," amesema.
Nyamhokya amesema ili waondokane na hilo Serikali ihakikishe inapata vielelezo halisi ili kukabiliana na watumishi watakaoingia kwa magendo.
"Mtumishi amebakisha mwaka mmoja kustaafu, amefukukuzwa kutokana na vyeti feki matokeo yake hana maandalizi yoyote na hakujiandaa kimaisha anaenda mtaani akiwa maskini,"amesema Nyamhokya.

No comments: