Advertisements

Sunday, July 2, 2017

Rais Magufuli Atoa ONYO Kwa Wanasiasa Waropoka, Awataka Polisi Wafanye Kazi Bila Kumuogopa Mtu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ametoa onyo kali kwa wanasiasa wanaotaka sifa za kisiasa kwa kushabikia waovu hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Rais amesema kuna watu wanashabikia maovu kwa kutoa matamko bila kuyapima madhara yake.

"Niwaombe wanasiasa wanaoshindwa kuzuia midomo yao, wanaosema kuwa hawa watu wameshikiliwa kwa muda mrefu, tunashindwa kujua hata kuna watu kule Marekani walikaa Guantanamo muda mrefu, katika hali hiyo kwanini usifanye watu wafikiri na wewe ni mmoja wao.Msitufanye tukafika huko"
"Kwanini hata siku moja mtu asijitokeze kulaani watu wanaouawa bila hatia kule. Lakini kwa kutaka sifa za kisiasa, mtu anatoka anasema hawa watu wako ndani muda mrefu, kuna ndugu zetu wanakufa kule...nataka polisi mfanye kazi yenu, hawa wanaoropoka waisaidie polisi, msiogope sura, awe na mwendo wa haraka, polepole au kukimbia, mkamateni ili kusudi aisaidie polisi akiwa kule ndani," amesema Rais John Magufuli na kuongeza;

"Juzi mtu amekamatwa na uniform 5000 za jeshi na inaonekana anahusika na hao walioko ndani, halafu unasema wamekaa muda mrefu, au na wewe ni miongoni mwa walioagiza hizo uniform za jeshi.

"Endeleeni kujenga heshima ya bandari, rushwa iwe ni marufuku, halafu muda pia... mtu akifika hapa akae muda mfupi na aondoke, hata kama anasafirisha pini ifike inapokwenda na sio ipotelee njiani

"Kuna vichwa 13 vya treni vimeshushwa hapa lakini havijulikani ni vya nani, tena inasemekana ni vibovu na TRL wamesema hawajaagiza na wala hawajasaini mkataba wowote.

"Hamkuuliza vya nani baada ya meli kuondoka ndio mnauliza, siku nyingine si watakuja kushusha hata na vifaru au makontena ya sumu?

"Sijui haya mavichwa mtafayanyia nini, lakini hili ni lazima lisemwe ili Watanzania wafahamu. Tutangulize uzalendo wa nchi yetu."

No comments: