ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 29, 2017

TIMU YA HEAD, INC DIASPORA 2017 MEDICAL MISSION ILIVYOKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA AFYA WA ZANZIBAR

Makamu  Waziri wa Afya Bi. Harusi Suleimani alikutana na timu ya msafara wa Madakatari wa Taasisi ya Diaspora ya HEAD, INC ilipokuwa hapa Zanzibar. Mkutano huo ulizungumzia mambo kadhaa kwanza kabisa ikiwemo kutoa shukuani kwa taasisi hiyo inayoundwa na kuongozwa na Diaspora wa Tanzania wanaoishi Marekani na Nchi nyingine tofauti. Makamu Waziri alisema ni jinsi gani serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inavyotambua na kuthamini msaada huo . Madawa yasiyoungua  Shilingi 1.4 Billioni za Kitanzania yalipelekwa Zanzibar na Taasisi hii yenye Makao Makuu yake nchini Marekani. Halikadhalia Waziri alisisitiza ni Jinsi gani serikali iko tayari kushirikiana na Diaspora katika nyanja ya afya na idara nyingine tofauti. 
Wakizungumza kama waanzilishi wa HEAD,INC na viongozi wa Msafara huu, Dada Asha Nyanganyi na Bwana Iddi Sandaly , walielezea ni jinsi gani walivyofarijika na mapokezi na ushirikiano walioupata kutoka Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Zanzibar Diaspora Desk, Ubalozi wa Tanzania Nchi Marekani na Taasisi za Afya na Mahospitali za Zanzibar, haswa Mnazi Mmoja hospital. Na wamethibitisha kuwa wamefarijika na kazi kubwa ipo na watarudi tena Zanzibar kila mwaka. Pia wazungumzaji hawa walitwashukuru wanadiaspora wote kwa michango yao ya hali, mali na ujuzi katika kufanikisha shughuli zote za HEAD, INC na haswa hii Medical Mission.

  Zawadi kutoka Ofisi ya Rais Zanzibar iliyokabidhiwa kwa HEAD,INC
  Zawadi kutoka Ofisi ya Rais Zanzibar iliyokabidhiwa kwa HEAD,INC
Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar Bi. Harusi Suleimani Akimkabidhi zawadi Ya "Paint" picha ya thamani ya kuchorwa kwa mkono mmoja wa Madaktari na Daktari kiongozi wa Msafari  Dr. Armel Semo.

      Makamu waziri wa Afya  Bi. Harusi Suleimani Akimkabidhi zawadi Ya "Paint" picha ya thamani ya kuchorwa kwa mkono mmoja wa Medical Team Members Kaka Yahaya Goronga anaeishi Kansas, USA.

    Makamu waziri wa Afya  Bi. Harusi Suleimani Akimkabidhi zawadi Ya "Paint" picha ya thamani ya kuchorwa kwa mkono mmoja wa Medical Team Members Dada Mariam Ganzo anaeishi Canada.



 



































No comments: