Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akisalimiana na Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayoajishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Bwana Said Al – Khemeir. Wa kwanza kutoka Kulia ni Mhandisi wa Taasisi ya Emirates Red Crecent Bwana Fateh Basel.
Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Taasisi
ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu
ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } inakusudia kujenga Nyumba Mpya za
Kisasa za Makaazi katika Wilaya tofauti za Zanzibar kwa ajili ya
Wananchi ambao Nyumba zao zimekumbwa na Maafa wakati wa msimu wa Mvua za
Masika uliopita.
Ujenzi
wa nyumba hizo unafuatia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa
kuzitaka Nchi, Taasisi na Mashirika rafiki ndani na nje ya Nchi
kusaidia kuunga mkono Wananchi walioathirika na Mvua hizo ambao wengine
wamepoteza kabisa Makaazi yao.
Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa
ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa
Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Bwana Said Al – Khemeir
alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Said
alisema Uongozi wa Taasisi yake ulifika Zanzibar kuangalia maeneo
yaliyoathirika na Mvua hizo na kuandaa Mipango itakayosaidia kuanzwa kwa
Mradi huo mkubwa utakaohusisha Wilaya zote zilizopatwa maafa hayo.
Alisema
Awamu ya kwanza ya mradi huo itaanza Kisiwani Pemba kwa ujenzi wa
Nyumba 30, zitakazokuwa na uwezo wa kuchukuwa Familia Mbili, Skuli yenye
Madarasa Saba na Maktaba yake, Hospitali, Msikiti pamoja na Maduka kwa
ajili ya wakaazi watakaoishi eneo husika.
Mwakilishi huyo wa
Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya
Kibinaadamu ya Emirates Red Crecent alisema Taasisi hiyo yenye kufanya
kazi chini ya ushauri wa Vyama vya Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu
Duniani imekuwa ikitoa huduma za kibinaadamu katika Mataifa mbali mbali
Duniani kutegemea na mahitaji ya Nchi husika.
Naye Mhandisi
Muandamizi wa Taasisi hiyo ya Emirates Red Crecent Fateh Basel
aliishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba maeneo
yatakayotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba hizo ni vyema yakawa
salama.
Mhandisi Basel alisema maeneo yatakayotengwa endapo
yatakuwa karibu na miundombinu ya Bara bara, Maji na Huduma za Umeme
yatasaidia kurahisisha mradi huo kukamilika kwa haraka ili kutoa faraja
kwa Wananchi waliothirika na Mvua za masika zilizopita.
Aliupongeza
ushirikiano wa karibu ulioonyeshwa na watendaji wa Wilaya na Mikoa
wakati wa ziara yao ya kukagua sehemu zilizoathirika na Mvua za Masika
pamoja na kuangalia baadhi ya maeneo salama yenye sifa na haiba ya
kujengwa kwa mradi huo.
Akitoa shukrani zake kwa Uongozi wa
Taasisi hiyo ya Emirates Red Crecent Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alisema kitendo kilichobuniwa na Taasisi hiyo
hakitolea faraja kwa Wananchi walioathirika na janga hilo pekee bali
hata na Serikali Kuu kwa ujumla.
Balozi Seif alisema atauagiza
Uongozi wa Kila Mkoa na Wilaya Visiwani Zanzibar kufanya utafiti na
uhakiki wa kuangalia maeneo yatakayoweza kuanzishwa miradi hiyo
itakayostawisha Wananchi waliokusudiwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar aliuhakikishia Uongozi huo wa Emirates Red Scecent kwamba
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itazingatia wazo hilo kwa ajili ya
kulitolea baraka zake ili Mradi huo uanze mara moja na kulet tija
iliyokusudiwa.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
21/7/2017.
Mwakilishi wa Taasisi ya Emirates Red Crecent ya Umoja wa Falme za Kiarabu Bwana Said Al – Khemeir wa Pili kutoka Kushoto akimfafanua Balozi Seif nia ya Taasisi yake kujenga Nyumba kwa ajili ya Wananchi walioathirika nja Mvua za Masika.
Mhandisi wa Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation Bwana Khamis Rasshid wa kwanza kutoka Kulia ambaye Kampuni yake ndio itakayosimamia Ujenzi wa Nyumba za Wananchi walioathirika na Mvua za Masika akifafanua jambo wakati Ujumbe wa Emirates Red Crecent upofanya mazunguma na Balozi Seif.
No comments:
Post a Comment