Na Mussa Mbeho,Tabora
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Dk Thea Ntara amewataka wanawake wajasiriamali mkoani humo kuchangamkia fursa mbalimbali za mikopo zinazotolewa na serikali ili kuweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuachana na Tabia ya kuwa tegemezi kwa waume zao
Dk Ntara ametoa wito huo katika uzinduzi wa jukwaa la wanawake kuinuana kiuchumi katika halmshauri ya Nzega Mji lililofanyika katika ukumbi wa pick poit Pub wilayani Nzega.
Amesema wanawake wote wajasiriamali mkoani humo wanatakiwa kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia halmashuri zao kwa kuunda vikundi mbalimbali ambavyo vitaweza kukopesheka kirahisi ili kuweza kuwasaidia kujikomboa na suala zima la umasikini kwa kuendeleza biashara zao.
Dk Ntana Ameongeza kuwa mwanamke hapaswi kukata tamaa katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo hasa kupitia biashara yake na kuwashauri kuongeza ubunifu ili kuweza kupata wateja wengi hali ambayo itasaidia kuza vipato vyao.
Aidha Dk Ntara ameyataka mabenki yote mkoani humo kutoa mikopo yenye riba nafuu ambayo itasaidia wanawake wengi kukopesheka na hatimae kujikomboa kiuchumi kupitia biashara zao.
Hata hivyo Dk Ntara amewaomba wanawake wote mkoani humo kuendelea kushirikiana na serikali katika mapambao ya dawa za kulevya pamoja na mimba za utotoni kwa kuwataja wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo ili sharia iweze kuchukua mkondo wake.
Nae Mkuu wa wilaya ya Nzega bwana Godfrey Ngupura amewashauri wanawake kuacha tabia ya kuwa waoga katika kutafuta fursa na badala yake wajiamini kwa kile wananchokifanya huku akiahidi kuendelea kuwa nao bega kwa bega katika kuwasaidia kujikwamua kiuchumi wanawake wote wilayani humo.
Kwa upande wake afisa Maendeleo ya Jamii wa halmashauri ya nzega mji Bwana Godson Halee amesema kuwa lengo la kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ni kuwawezesha wanawake kukutana pamoja na kujadili fursa walizonazo katika suala zima la kujikwamua kiuchumi huku akibainisha kuwa katika msimu mpya wa fedha wa 2017/2018 halmashauri hiyo imetenga jumla ya shilingi milioni 124 ili kuweza kuvikopesha vikundi vya wajasiriamali wanawake na vijana katika halmashauri hiyo.
Uzinduzi wa jukwaa hilo la wanawake kuinuana kiuchumi Umekwenda sambamba na uchaguzi wa viongozi wa nafasi ya mwenyekiti.katibu na mtunza hazina ambao watasaidia kusimamia shughuli zote za jukwaa hilo katika halmashauri ya Nzega Mji.
No comments:
Post a Comment