Advertisements

Friday, July 14, 2017

WAZIRI MKUU AUPONGEZA UONGOZI WA NHC KWA UTENDAJI

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanganga, wakati alipo simama, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amkabidhi Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambi mipira,  wakati alipo simama katika kijiji cha Nanganga,  akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. 
 Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambi akiwa na Mbunge wa Masasi  Rashid Chuwachuwa (Kushoto) na Diwani wa Kata ya Ndanda Costancia Bernad, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipo simama katika kijiji cha Nanganga,  akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Wananchi wa kijiji cha Nanganga wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  wakati alipo simama katika kijiji hicho,  akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.
 Wananchi wa kijiji cha Mtama wakishangilia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,  wakati alipo simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo,  akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Mtama,Nape Mnauye alipo simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo,  akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtama, wakati alipo simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo,  akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC),wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye Julai 13, 2017.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akikata utepe wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (kutoka kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye, Diwani Kata ya Mnolela Omar Liveta, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) kutoka kulia ni Meneja NHC Lindi Gibson Mwaigomole, Meneja NHC Mtwara Nehemia Msigwa, Mkuu wa Mkoa Lindi Godrey Zambi Julai 13, 2017.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akikagua wakati kifaa katika Zahanati ya Mnolela, baada ya kuifungua, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na wananchi wa Mnolela mara baada ya kuifungua Zahanati hiyo iliyopo katika Kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani Lindi kwa muda mfupi. 




Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa mwezi Machi, 2017 na sasa tayari kimekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na wa jirani. 


Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo jana jioni (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na NHC. 

Alisema ujenzi wa zahanati hiyo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa kusogeza huduma karibu kwa wananchi wake. 

“Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto za mbalimbali zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.” 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ulisimamiwa na NHC na umegharimu sh. milioni 65.5. 

“Shilingi milioni 15 zilitolewa na Rais. Dkt. Magufuli, sh. milioni 10 zilitolewa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye, NHC ilitoa sh. milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa halmashauri.” 

Awali Mbunge wa jimbo la Mtama, Mheshimiwa Nape alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa katika mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo. 

Mheshimiwa Nape alisema zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakati wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine wanaoishi kwenye maeneo yaliyo jirani na kijiji hicho. 

IMETOLEWA NA: 

OFISI YA WAZIRI MKUU, 
IJUMAA, JULAI 14, 2017

No comments: