ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 24, 2017

IGP SIRRO AFANYA UTEUZI WA KAIMU KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR NA KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA



                       Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                      Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
                       Simu : (022) 2110734                                                                                      Makao Makuu ya Polisi,
                       Fax Na. (022) 2135556                                                                                                             S.L.P. 9141,
                               DAR ES SALAAM.
                                                                  

24/08/2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Juma Yusuf Ally kuwa Kaimu Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Uteuzi huo unafuatia kustaafu kwa aliyekuwa kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdani Omari Makame kwa mujibu wa sheria baada ya kutimiza umri wa miaka sitini (60).

Kabla ya uteuzi huo DCP Juma alikuwa ni Mkuu wa Utawala na Fedha Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.

IGP Sirro pia amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  (SACP) Lazaro Mambosasa kuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Kabla ya uteuzi huo, SACP Mambosasa alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi  (SACP) Neema Mwalimu Mwanga anakwenda Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.


IGP Sirro pia amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Gilles Bilabaye Mroto kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na  Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Emmanuel Lukula kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke.

Kabla ya uteuzi huo, ACP Lukula alikuwa Afisa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Mbeya.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuendela kushirikiana na Jeshi hilo kwa kufichua taarifa za uhalifu na wahalifu ili kwa pamoja tuendelee kuiweka Tanzania salama.


Imetolewa na:
Barnabas David Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
S.L.P 9141
Dar es Salaam

www.policeforce.go.tz                 www.facebook.com/tanpol      www.twiter.com/tanpol  

No comments: