Majaji wa Mahakama Kuu nchini Thailand wametoa kibali cha kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Yingluck Shinawatra mwenye umri wa miaka 50.
Mahakama hiyo imefikia maamuzi hayo baada ya waziri huyo kutohudhuria mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili ya makosa ya uhalifu wa kuzembe kazini kwa madai kuwa anaugua ugonjwa wa vertigo.
Hata hivyo kiongozi huyo amekanusha makosa hayo ya kuzembea kazini yanayohusiana na mradi wa mpunga wa gharama ya mabilioni ya dola ambayo yamepotea.
Moja ya ulinzi uliowekwa wakati wa kesi ya Yingluck Shinawatra nje ya Mahakama
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, limesema Mahakama imefikia maamuzi hayo ya kutoa kibali cha kukamatwa kwake kwani anaweza kuikimbia nchi hiyo muda wowote. Wakati huo huo Mahakama hiyo imeipiga chini dhamana ya dola 900,000 ambayo alikuwa ameiweka waziri Shinawatra wakati wa kuanza kwa kesi hiyo.
No comments:
Post a Comment