Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) Bw. Kailima Ramadhani (Kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
(kushoto) alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi eneo la kuhifadhia
Mashine za BVR. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na
Bunge), Maimuna Tarishi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitazama moja ya Daftari la Wapiga Kura
alipotembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam. Katikati
ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani na Kushoto ni Afisa TEHAMA wa
Tume Bi. Mwamvita Solo.
Afisa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw.
Julius Kobelsiki akitoa ufafanuzi kuhusu Mashine ya kuandikisha Wapiga Kura ya
BVR kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye
Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya watendaji na
watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kuhitimisha ziara yake
katika Ofisi za Tume jijini Dar es salaam. Kulia kwake Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi na Mkurugenzi wa Uchaguzi
Bw. Kailima Ramadhani (kulia).
Na. Aron Msigwa - Dar es slaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira
na Watu Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuendelea kusimamia
matumizi bora ya rasilimali inazopewa na Serikali na kuzitaka taasisi nyingine
za Serikali kuiga mfano huo.
Mhe. Muhagama ameyasema
hayo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea ofisi za Tume ya Taifa
ya Uchaguzi kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Bunge kupitia Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora iliyoridhia Bunge lipitishe fedha
kiasi cha shilingi bilioni 10 kuiwezesha Tume kufanya maandalizi ya Uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini .
Akizungumza na watendaji na
baadhi ya watumishi wa Tume amesema kuwa ameridhishwa na utendaji kazi wao na
namna Tume ilivyojipanga kutekeleza jukumu la uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura kuelekea uchaguzi ujao wa mwaka 2020 kwa kuwa na mpango Kazi,
unaochambua na kubainisha mahitaji muhimu yanayotakiwa, lini na wapi ili kazi
hiyo iweze kufanyika kwa umakini.
“ Naipongeza sana Tume kwa
kuendelea kufanya vizuri , nimegundua kuwa imejipanga vizuri kutekeleza
majukumu yake ambayo yameainishwa Katika Katiba, kwa niaba ya Waziri Mkuu nimekuja hapa na timu
ya watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuangalia utekelezaji wa maagizo ya
Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bora walioridhia Bunge lipitishe
fedha shilingi Bilioni 10 ili kuiwezesha kufanya maandalizi ya Uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura” Amesema.
No comments:
Post a Comment